Thursday, May 7, 2020

JUST MY THINKING CALL.



JUST MY THINKING CALL.


Am trying to think about the future of HR after Corona. According to ILO, every 15s one employees die because of accidents in the working place. More than 374 million accidents occur in the working place in the world per year. Furthermore, in developing country around 881280 people get disease from their job. All these happened before tragedy COVID-19 accident. Am trying to think about how the situation today? Am trying to think how HR situation in COVID-19? Are they safe? If not, how production have been affected? What is the response from their employers? How about their job security? Am trying to think how the situation of HR in developing country today? Is there any relationship between being health and production? Am thinking how many people have died because of COVID-19? So sad…but it is my thinking only don’t worry. Am just thinking only. We shall overcome! Together we can! Everyone is passing through this tough time. It is a balance game for both rich and poor nation, week and strong industrial. Let us prepare for the new chapter. Get ready for the new economic competition. The world will be more giant than today. Wishing all the best! Stay safe! You are the most potential HR! Avoid Corona. Please, you can share to me how do you think and feel in this tragic time? Remember you are the winner. By James Kalimanzila (Hungry Learner)

Friday, April 10, 2020

Employee's Security and Safety in an organisation.



This short video demonstrates the necessity of employee's safety and security in their working places particularly in the era 4.0. Recently, there is greater economic competition among organizations and nations due to the development of Technology, Creativity, and Innovation. Therefore, every organization wants to have strong and healthier employees toward high organization production. Please visit my YOUTUBE channel. Don't forget to SUBSCRIBE (James Kalimanzila HRM Mentor) for more video and knowledge sharing..comment, discuss and advise.

Stay home...wash your hand..Avoid Corona be a Healthier and energetic HR for more production.


Wednesday, April 1, 2020

Employees Onboarding (EO)


Currently, Onboarding is a key and principal tool in any missioned and planned organization. Moreover, the development of technology, innovation, and creativity has increased the necessity and application of Onboarding more than before. New employees need new skills and knowledge to suit new organizational culture and technology. Likewise, socialization and friendly cooperation is more vital to fulfill this. Furthermore, every organization today needs to have a new model, style, and approach to undergo onboarding depending on their environment and technology. A new employee may need only a few basic important things in their first onboarding such us socialization, responsibility, and care this will motivate them to apply these skills for the betterment of the organization but later they will need a good salary, training, technology among other. However, onboarding today has dynamic approaches in passing skills to new employees.

All in all, Onboarding, is also referred as organizational socialization, it is a management verbiage initial created in the 1970s that refers to the mechanism through which new employees acquire the necessary knowledge, skills, and behaviors in order to become effective organizational followers and insider.

 Thank you very much. Stay safe, wash your hands, avoid unnecessary meetings. Avoid Corona. You are a very potential Human Resource in an organization, family, community, national as well as the world still need you.

Please share your understanding on Employees Onboarding (EO)

By Hungry Learner.

Wednesday, March 25, 2020

HADITHI ZA KINDIJA



HADITHI ZA KINDIJA

Kitabu hiki ni kitabu cha kwanza katika mfululizo wa hadhithi za Fasihi simulizi zenye utamu na mtiririko wa kuvutia toka kwa Ndugu James Kalimanzila. Kutokana na vijana wengi leo kutokuwa na utambuzi wa mila na tamaduni zetu za kitanzania wamejikuta wakiuvaa usasa na kutembea chini ya mwamvuli wa utandawazi na kuhisi hapo ndio mwisho wa maisha.
Maisha huwa hayawezi kwenda mbele bila ya kukumbuka yalikotoka. Ndio maana vijana wengi hata waliosoma hawasikii furaha ya moyoni kwa sababu mila na desturi zao ndizo zilikusudiwa kuwapa furaha mioyoni mwao. Hapa mwandishi amekusudia kuwakumbusha japo kwa uchache baadhi ya mila na desturi za kisukuma kwa wale walioanza kusahau au kwa wasio na utambuzi kabisa na mila na desturi hizo.
 Aidha mwandishi wa kitabu hiki ameamua pia kutia kalamu yake katika uandishi wa kazi za Fasihi kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo kwenye kazi za Fasihi. Mahitaji haya ni pamoja na kuinua kiwango cha ujuzi wa lugha na uwezo wa kusoma na kufahamu. Ni dhumuni mahususi la mfululizo wa vitabu hivi kuimarisha maadili ya wasomaji wake kwa kuinua ubunifu, udadidisi, bidii, uaminifu, utiifu na kuhuisha mapenzi ya dhati.
Hadithi zote zimeandikwa kwa njia ya kuwavutia na kuwapendeza wasomaji pamoja na kuwapa mafunzo yafaayo. James Kalimanzila ambaye ni mwandishi na mtunzi wa kitabu hiki amewahi kutunga na kuandika kazi nyingi kama: Flip-flop of labour shortage pamoja na Palaysed digital economy. Aidha katika kuandaa kazi hii ameshirikiana na ndugu Godlove Dismas Ngowella, Mwalimu na mtaalam wa fasihi ya Kingereza.
HADITHI 1. MZIMU WANGU.
Kulikuwa na kijana aliyejulikana kwa jina la Dongwe, kijana huyu alizaliwa katika kijiji cha Kanyaga kilichopo mashariki mwa Wilaya ya Kahama. Kijiji cha Kanyaga kina madhari ya milima ya mawe makubwa, mapango, misitu minene, mito yenye kina kirefu na mabwawa ya maji. Wanakijiji wa Kanyaga walikuwa wafugaji wa mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda. Walikuwa wakijishughulisha pia na shughuli za kilimo cha mazao kama vile mahindi, maharagwe, njugu mawe, karanga, mihogo, miwa na mpunga.
Wanakijiji wa Kanyaga walikuwa wakiamini katika mila na desturi za Uswega ambazo walizirithi kutoka kwa mizimu ya babu zao. Katika kuhakikisha kuwa mila na desturi za kijiji hiki zinatunzwa na kurithishwa kwa vizazi vijavyo kulikuwa na desturi ya kumrithi uongozi kiongozi aliyefariki. Vigezo vya urithi vilitaka kijana wa kiume, kipenzi cha marehemu baba yake na kipenzi mizimu pia.
Nchemu, baba yake na Dongwe ndiye aliyekuwa kiongozi kwa miaka Zaidi ya 100. Nchemu alirithi uongozi huu kutoka kwa baba yake aliyeitwa Doi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 115. Kwa ufupi familia ya Dongwe ndio ilikuwa familia ya kitemi pale kijijini. Familia ya kitemi ndiyo ilikuwa ikihusika na kwenda kuongoza ibada za matambiko ya kimila kwa ajili ya kuomba Amani, mvua, kutoa mikosi kama ya kuvamiwa na wadudu waharibifu wa mazao aina ya nzige na mabuu.
Kijana Dongwe alipendwa sana na wazazi wake hasa baba yake huku akiwa ni kijana pekee wa kiume aliyebakia baada ya kaka yake kufariki kwa kula uyoga wa sumu. Wabeba mikoba, waliokuwa wakimsaidia Ntemi, walihakiki kuwa Dongwe ndilo chaguo la mizimu kwa sababu licha ya kula uyoga wenye sumu wakiwa pamoja na kaka yake, kijana huyu hakudhurika hata kidogo. Hii ilisemwa kuwa ni ulinzi madhubuti wa mizimu juu yake kwa sababu ndiye aliyepaswa rithi mikoba ya baba yake.
Dongwe alipotimiza umri wa miaka 10 Baba yake alifariki dunia kutokana na magonjwa ya uzee yaliokuwa yakimkabili, kwani alikuwa amefikisha umri ya miaka 130. Msiba huu ulikuwa pigo kubwa kwa kijana Dongwe, alilia usiku na mchana akifirikiri labda machozi mengi yangeweza kuwa tiba ya baba yake kuamka. Haikuwa vile alivotaka yeye maana siku ya tatu baba yake alifukiwa na kifusi cha udongo na kuwekewa maua juu ya kaburi na baadaye kumwangwa damu ya kondoo juu ya kaburi lake.  Alikumbuka namna baba yake alipotuma walinzi wake waende kumchagulia vazi zuri na viatu vya makata mbuga, magurudumu ya gari, siku ya gurio. Vazi na makata mbuga vilikuwa zawadi ya mwisho ya baba yake na ndivyo alivyokuwa amevaa wakati wote wa msiba wa baba yake.
  Kijana Dongwe alisikitika sana hasa alipokumbuka namna alivyopendwa na Baba yake na namna yeye mwenyewe alivyompenda baba yake. Lakini pia alibaki kuwa na huzuni Zaidi kiasi cha kukosa hamu ya kula na usingizi kumpaa mara baada ya kugundua kuwa yeye ndie aliyetakiwa kurithi mikoba ya mila za Uswega. Aliwaza sana angewezaje kuwaongoza watu waliomzidi umri. Sauti yake ilikuwa ya kitoto asingeweza kuongea kwa amri kama baba yake. Angewezaje kuiuliza mizimu kuleta mvua na amani kwa kijiji chake. Mawazo kama hayo na mengine yalimtafuna sana kijana Dongwe.
Baada ya mwaka mmoja kupita, ndipo watu waliruhusiwa kuanua matanga- yaani kumaliza msiba wa Ntemi wa kijiji. Siku ya mwisho ilikuwa sherehe kubwa sana ambayo haijawahi tokea kijijini hapo. Ng’ombe walichinjwa mpaka walaji wa chibulanga wakachoka kukinga damu, vinu vilikesha vikitwanga mpunga na pombe ilikorogwa kwenye mapipa ya kutosha kiasi cha kuwalevya walevi hata kabla hawajaanza kuitumia. Ngoma kubwa kwa ndogo zilipigwa mpaka vijiji vya jirani vikajialika kuja kushuhudia nini kikichokuwa kikifukuta kwa majirani zao.
 Wakati sherehe ikiendelea, wazee wa kijiji walikutana ajili ya kupanga safari ya kwenda kumtawadha Ntemi kijana Dongwe. Maana sherehe iliyofanywa ilikuwa sherehe ya kuiaga mizimu ya Nchemu na sasa kijiji ikilikuwa kinaelekea kosa mizimu ya kukiongoza. Hivyo kwa sababu kimila mizimu ya Nchemu licha ya kuagwa siku ya leo ingeondoka kesho yake majira ya jioni. Hivyo basi desturi zilihitaji mizimu mipya kukabidhiwa kijiji kutoka kwa mizimu ya zamani. Kuchelewesha makabidhiano haya ni kuikaribisha mizimu mibaya ya magonjwa, vifo na mikosi kwa kijiji chao.
Wazee walikubaliana kwenda kwa tambiko majira ya alfajiri na wangedumu huko kwa muda wa siku 10 mpaka mizimu itakapompa kibali Ntemi mpya kuingia katika utawala. Wazee waliandaa vyakula na wanyama kwa ajili ya chakula chao na kwa ajili ya tambiko kubwa la siku ya mwisho. Walitawanyika wakikubaliana wangekutana nyumbani hapo kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea msitu wa matambiko. Wanakijiji wengine waliendelea na sherehe wakila na kunywa na kucheza ngoma kwa furaha usiku kucha.
Alfajiri kabla ya jogoo kuwika wazee wa kijiji na wasaidizi wa Ntemi wakapakia vyakula vyao migongoni mwa punda, na wengine wakatangulia na mifugo iliyochaguliwa kwa ajili ya tambiko na nyama. Safari ya kwenda katika msitu wa tambiko ikaanza. Wazee na vijana wote walitembea kwa haraka kwa miguu yao, Dongwe pekee ndiye aliyebebwa kwenye kiti kilichobebwa juu na walinzi wa Ntemi. Hofu kubwa njiani ilikuwa ni kwa kiumbe bundi kulia usiku ule. Kwa mila zao kama bundi angelia tu safari ilikuwa inaharishwa, maana mlio wa bundi ni uchuro, na sherehe kule kijijini inangenda kuanza upya ili mizimu isiondoke.
Kwa bahati njema ndege bundi wenye uchuro mwingi walikuwa watulivu mpaka msafara ukafika katika msitu mnene wenye uvuli wa kiza kinene. Hakukuwa na mtu aliyediriki kupita au kukata kuni katika msitu huu. Msafara huu tu ulioingia sasa nywele zao za visogoni zilikuwa zimesimama kwa hofu kuu. Kiongozi wa wazee aliomba vijana walete kondoo na akachinjwa chini ya mti mkubwa, ambao ulikuwa unatisha sana, kama ishara ya Amani.
Kijana huyu alifanyiwa sherehe ya kurithi mikoba hiyo ambayo ilifanywa kwa siku 10 mfululizo, msitu wa tambiko pia ulikuwa ni msitu wenye wanyama wakali kama vile nyoka wenye sumu kali koboko, chatu, simba, fisi, chui na kadhalika. Licha ya wanyama hawa hatarishi kwa maisha ya Dongwe na wengine, sherehe hizi pia zilitakiwa zifanyike usiku wa kiza totoro huku wahusika wakiwa wamevua nguo zote na kufumba macho yao huku muhusika peke yake ndiye aliye kuwa na idhini ya kufumbua mambo yake.
Koboko aliwika kama jogoo kila ilipokaribia alfarijiri, fisi walikuwa wakisikika wakicheka kila baada ya jua kuzama na miungurumo ya simba ilikuwa haina muda maalumu. Kijana Dongwe alijuta kuzaliwa kwani alikuwa na hofu kubwa juu ya sauti za kutisha za wanyama hao na alijionea mambo mengi makubwa ambayo hakuweza kuyawaza wala kuyafikiria huko porini. Baada ya siku tatu polini huku chakula chao kikuu kikiwa ugali na nyama alijikuta akiwa mtu mwenye mawazo mengi sana.
Siku zilikuwa zinaenda polepole mno kwa akili ya kijana Dongwe alitamani azisogeze mbele ili atoke kwenye lile balaa lakini wapi, masaa yalikuwa kumi na mbili mchana na usiku hali kadhalika. Siku ya tano baba yake alimtokea kwenye jozi za usiku huku akimpa moyo wa ushujaa na ujasiri. Alimuhakikishia kuwa vitu vyote vingenda salama maana yeye ndiye aliyewakemea bundi kuwika usiku wa safari yao kuja kwenye tambiko. Dongwe alijikuta akipata ujasiri mkubwa na kujikuta mwenye furaha na nguvu japo urithi huu hakuupenda kabisa katika maisha yake alijiapiza moyoni mwake kuusaliti na kutoa elimu pale atakapokua mtu mzima kwani hakufurahishwa na mambo aliyojionea msituni.
Siku ya kumi ilipowadia ngoma zilianza kupigwa kwa nguvu huku kiongozi wa wazee akinyunyuzia damu ya kondoo kwenye mti wa tambiko kwa kutumia mkia wa simba. Dongwe akaitwa akawekwa katikati ya wazee akawekewa mikono yote kichwani kama ishara ya kumbariki. Ngoma zilizidi rindima msituni pale. Dongwe aliombwa kusogea karibu na mti wa tambiko. Alisimama kwa ujasiri na kwenda kusimama mbele ya mti wa tambiko.
Radi zilipiga, ngurumo zikarindima msituni pale. Watu wote wakiwa tupu kama walivyozaliwa na wamefumba macho yao maana atakayefumbua macho ni lazima apigwe radi au ang’atwe na koboko. Aliyekuwa anaangalia muda wote huu ni kijana Dongwe. Mara kuhamaki anamuona koboko akimuangalia usoni huku ulimi ukiwa unatoka na kurudi tena ndani. Dongwe akajipa ujasiri akamuangalia koboko kwenye macho yake. ‘‘Macho ya koboko ni mazuri na huwa kama anayarembua hivi lakini sumu yake inatumia muda mfupi sana samba mwilini na kumuua mtu hata kabla ya kupatiwa dawa,’’ Dongwe alikumbuka maneno ya mama yake.
Mara ghafla koboko akatoweka! Dongwe hakuamini macho yake, akayafikicha kwa mikono yake kuangalia vizuri, patupu! Wakati akihamaki mwanga mkali wa radi ukamulika miguuni kwake. Wakati bado akihamaki na kubaha ikatokea fimbo pale ulipomulika mwanga wa radi. Sauti nzito ya kuamrisha ikasikika ikimwambia, ‘‘Solaga’’ bila ubishi akainama na kwa kutumia mikono miwili akaiokota ile fimbo. Alipomaliza tu kuiokota ile fimbo akaanguka chini, puuu. Ngoma zikaongeza mlio wake radi na ngurumo vikazidi kwa muda. Dongwe akawa akitapatapa pale chini huku povu jeupe likimtoka mdomoni.
Baada ya muda kama masaa matatu, Dongwe akaamka. Akaunyoosha mkono wake juu mara radi na ngurumo vikatulia tuli. Akaonekana kuwa na nguvu za ajabu sana. Akaongea kwa sauti nzito kama muungurumo wa simba, ‘Nipeni kondoo mzima na kisu.’’ Alipoletelewa akamfunga miguu kwa kamba moja kisha akamtoboa shingo yake na kuanza kumnyonya damu mpaka kondoo alipokufa.
Dongwe akawaamuru wote kufumbua macho. Na wote wakafumbua macho. Akaamuru kuni zisogezwe, kuni zikaletwa mpaka akaamuru kwa mkono kwamba zimetosha. Akanyonya fimbo yake kwenye kuni mara moto ukawaka. Watu wote wakaogopa sana. Akawaamuru kuchinja wanyama wote na kumkabidhi damu ambayo aliinywa yote bila kusaza hata tone.
Dongwe ameshakuwa Ntemi kamili sasa akamuoka kondoo mmoja na akamla mpaka alipommaliza. Akawaamuru wazee kula haraka hara na wakatii. Ntemi Dongwe akasema haya mvua njoo na unyeshe haswa mpaka tutakapofika nyumbani. Ghafla mvua kubwa isiyo na ngurumo wala upepo ikaanza kunyesha. Wazee wakabaki wakishangaa lakini Ntemi Dongwe akatoa amri kwa sauti ya simba, ‘‘Tujagi baghosha.’’ Wazee kwa vijana wakawa wakitetema tu mbele zake. Safari ya kurudi kijijini ikaanza huku Dongwe akibebwa juu na ngoma zikilia kwa sauti ya juu Zaidi.

HADITHI 2: KASHINDYE MKAUSHA MAJI.
Wananchi wa kijiji cha Kanyaga walikuwa ni kati ya wanakijiji walioonewa wivu sana wa wanavijiji wengine waliowazungukuka kwa sababu ya Amani, upendo na furaha kati yao. Walikuwa sio watu wa kutaka makuu, walikuwa wakitafuta Amani hata na vijiji vya jirani ili waweze kuishi vyema. Kitu ambocho kinaleta furaha kuna wakati pia kinaweza leta huzuni kwa kiwango sawa na furaha mpaka kikakuchanganya.
Hata hivyo watu wa kijiji cha Kanyaga walikuwa na mila na desturi zao walizozishikilia kweli kweli bila kufanya jaribio lolote la kuzipindisha. Watoto waliokuwa wakizaliwa kwa kutanguliza miguu au makalio, Makashindye, na wale waliokuwa wakisababisha wazazi wao kufariki wakati wa kujifungua walikuwa ni mikosi kwa familia na kijiji kizima. Mosi walikuwa wakiaminika kuwa wanakausha visima na mabwawa ya maji ya kijiji. Pili walikuwa wakisemekana kuzuia maendeleo na mafanikio kwa kila kinachofanyika pale kijijini.
Ilitokea mwaka mmoja wakati wa utawala wa Nchemu. Kulikuwa na shida kubwa sana ya maji kijijini Kanyaga na vijiji vya jirani. Kwa sababu kijiji cha kanyaga kilikuwa bondeni basi vijiji vingine vilikuwa vikileta zawadi ya mazao na mifugo kwa ajili ya kupewa maji ya matumizi yao wenyewe na mifugo yao. Ilifika kipindi maji yakawa yanapungua kwa kasi sana. Kati ya mabwawa matano ya maji yaliyokuwa yakitegemewa na kijiji kizima yalikauka na kubakiwa na bwawa moja tu tena lenye maji machafu.
Wazee wakiongozwa na Ntemi Nchemu wakaenda kwa ajili ya tambiko ili kukinusuru kijiji chao na vijiji vya jirani pia kutokana na shida ya maji. Baada ya tambiko mizimu ililaumu sana wanakijiji kuendelea kukaa na mtu anayerudisha nyuma mafanikio ya kijiji na juhudi za mizimu kukineemesha kijiji. Mizimu ilidai kuwa kuna kashindye anayekausha maji kila akienda kuchota ndoo moja anaondoka na mapipa Zaidi ya hamsini ambayo mizimu yake huenda kuyamwaga jangwani. Kazi ikatolewa ya kumtafuta kahindye miongoni mwa wanakijiji wa kijiji cha Kanyaga.
Baragumu kubwa iliyotengenezwa kwa pembe la nyati likapulizwa ili kuwakusanya watu chini ya mwembe mkubwa likalia. Na lamgambo likilia ujue kuna jambo. Watu wote wakakusanyika na kuwa watulivu kusikia kile walichoitiwa. Wengi alijua ni suala la maji ila hawakujua maji yangeweza kuwa na matokeo ya kushangaza hivi. Ntemi alisimama na kuwaeleza wanakijiji kuwa kuna kashindye na ajitokeze maaa ndiye chanzo cha tatizo kubwa la maji pale kijijini. Kwa alivyofura mfalme kila mtu alijua kifuatacho ni kifo. Hivyo hakuna aliyejitokeza.
Mpango wa kuongezwa kwa kina cha bwawa ukatangazwa ukiwa na lengo la kumpata kashindye. Basi vijana wa kiume wakavua fulana zao wakabaki vifua wazi wakaanza kuchimba kuongeza kina cha bwawa. Walipoyakaribia maji wakatolewa vijana wote akawa anaingia mmoja baada ya mmoja. Alipoingia kashindye mambo yakamchachia kila akichimba maji yanakimbilia chini. Wenzake walichimba mpaka wakayakuta maji alipoanza yeye maji yote yakakimbilia chini Zaidi. Chimba, chimba, chimba na wewe, wapi! Kashindye akawekwa chini ya uangalizi maalumu nyumbani kwa kiongozi wa sungu sungu wa kijiji.
Vijana wengine wakaendelea kuchimba ili kuongeza kina cha bwawa. Maji yalipatikana kwa wingi sana na watu wakaruhusiwa kuchota maji yale wala hayakupungua tena. Lakini kila mmoja akawa akishangaa kwa nini mwanakijiji mwenzao aliyeitwa Marando leo ameonekana kuwa ni kikwazo kwa kijiji kizima. Wote walikuwa wakimfahamu sana na hata nyumbani kwa wazizi wake palikuwa panajulikana. Familia yao hawajawahi kupatikana na tuhuma za uchawi au wizi hata siku moja. ‘‘Leo umekuchaje kwa Marando jamani?’’ Walishangaa sana.
Wazee walikutana kwa ajili ya kutafuta watu ambao wangeenda timiza adhima ya mizimu ya kumuua kashindye katika msitu wa tambiko tena kikundi hiki kilipendekezwa kuwa kiwe ni kikundi endelevu kwa ajili ya kutekeleza adhabu ya kifo kwa makashindye, wanaosababisha vifo vya wazazi wao na wachawi wa kijiji kile. Sangijo, Mtupa, na Kitinde ndio waliochaguliwa kuwa kikundi cha kukomesha mikosi pale kijijini kwa sababu ya ukubwa wa miili yao hivyo wasingeshindwa kitu.
Vijana hawa waliitwa kwenye baraza la wazee na kupewa maelekezo na kwamba baada ya kufanya tukio lile wazee wangewafanyia matambiko ili wasijedhurika. Maana inaaminika mtu akitoa uhai wa mtu mwingine basi lile jinamizi la marehemu linamuwinda muhusika mpaka litakapolipiza kisasi cha roho ndipo linapumzika au hata kuendelea kutoa roho zingine za wanafamilia mmoja baada ya mwingine. Vijana hawa watatu licha ya kwamba walikuwa na misuli na maumbo makubwa ya miilii yao lakini mioyo yao ilikuwa na uoga mno. Ila hawakukataa wito wa wazee.
Walipanga jioni ile wakamfunge kwenye gunia kubwa ili asiwatambue. Maana kiongozi wa sungu sungu alikuwa amemweka Marando kwenye chumba chenye kiza sana, hivyo Marando hakuwa akijua kuwa nje ni usiku au mchana. Walitafuta gunia kubwa la katani, Kamba nzuri za katani, mapanga matatu yaliyonolewa vizuri na shoka moja. Kama mtu angekutana nao alfajiri angejua wanaenda kuchinja ng’ombe mahali. Kwa ukimya na huzuni kubwa walikula chakula chao cha jioni ili wasije wakazidiwa nguvu wakati wa kutimiza maelekezo waliyopewa na wazee wa kijiji.
Vijana kwa ujasiri wakakiingia chumba alichokuwamo Marando. ‘‘We ni nani?’’ Marando aliuliza kwa hofu. Akastushwa na ngwara aliyopigwa akaanguka kama gunia la viazi vibovu. Hajakaa sawa akajikuta ndani ya gunia, akanyanyuliwa mzega mzega. Hofu ikamjaa Marando akaangua kilio kikuu lakini kila aliyesikia kilio chake alifunga mlango ili nae aangue kilio chake akiwa ndani ya nyumba yake. Kila mtu alimpenda Marando pale kijijini lakini amekuwa akitembea na bahati mbaya ndio maana hata wasichana walikuwa wakikataa kuolewa nae bila sababu za msingi. Kwa hiyo watu walilia kwa sababu ya kumpoteza mtu ambaye walikuwa wakikusudia labda angepata furaha baadae lakini wapi.
Kilio cha Marando kikageuka kuwa mayowe yaliyozidiwa nguvu na unene wa misitu waliyokuwa wakiiipitia. Wazazi wa Marando walijiondokea kijijini hapo siku ile ile mototo wao mpendwa wa kiume aliposemwa kuwa ni mkosi wa kijiji kizima. Hawakuweza kuvumilia mototo wao aliyeyekuwa na machungu ya kukataliwa na wasichana wa kijijini hapo eti leo anakuwa mkosi wa kijiji na anatakiwa kuuuwawa bila maelelezo yanayojitosheleza. Hata hivyo miungu huwa haihojiwi ndio maana waliamua kuhama kijiji cha Kanyaga.
Walipokaribia msitu wa tambiko simba akaunguruma mara tatu mfululizo. Marando akanyamaza na kujikuta anajisaidia haja dogo. Vijana wale watatu baada ya kuona wanalowanishwa na mkojo tena wa mtu mzima wakamshusha chini kimya kimya, wakaoneshana ishara kwamba Mtupa ampige shoka la shingo na warudi ili wasije wakadhuriwa na simba. Mtupa hakuwa mbishi akachukua shoka akalinyanyua wima juu ili alishushe na kutenganisha kichwa na kiwiliwili cha rafiki yake wa tangu utotoni.
Shoka likagoma kushuka, machozi yakaanza kumtoka wenzake wakamuonesha ishara ashushe shoka inapoonekana kuwa ni shingo. Mtupa akaangua kilio kwa nguvu akasema ‘‘siwezi kufanya hivi sitaweza kuishi kwa Amani abadani.’’ Alipomaliza kuongea tu. Marando akaifahamu sauti ya rafiki yake kipenzi. Marando akamwambia, ‘‘Mtupa rafiki yangu naomba unisaidie, unanifahamu mimi na matatizo yangu naomba uniokoe hapa tu.’’ Sangijo na Kitinde nao wakaanza kulia kwa uchungu mno pamoja na rafiki yao.
Wakajikuta wanamfungulia na kumwambia ‘tunaokoa maisha yako ila maisha yetu yatakuwa hatarini mpaka kufa kwetu endapo utaonekana na mwanakijiji yeyote wa Kanyaga.’ Wakamuomba akimbimbie aende kijiji cha mbali kwa ajili ya kujitafutia maisha huko. Marando hakusubiri neno lingine alifukua mbio kama anakimbizana na malaika wa kifo.
Mtupa, Sangijo na Kitinde wakarudi kijijini wakiwa na huzuni katika nyuso zao. Wazee wakawapa kila mmoja ng’ombe ishirini na mbuzi kumi. Na kuwaahidi kama wangeanza kujisikia hatia au mikosi basi waombe tambiko la wazee. Kijiji kizima kilijaa na huzuni isiyosemekana kwa muda usiojulikana. Hata wale wasichana waliomkataa Marando walimuonea huruma sana. Huzuni ziliisha kwenye nyuso za watu lakini zikabakia kwenye mioyo yao

HADITHI 3: MALKIA KASHINDYE
Utawala wa Ntemi Dongwe ulikuwa utawala haswa. Kila mtu aliweza kusema Dongwe alikuwa na mizimu yenye nguvu na makini kuliko watangulizi wake waliomtangulia yaani baba yake na babu yake. Ntemi Dongwe kijana mdogo mwenye mipango mikubwa na madhubuti isiyotiliwa hata lepe la wasiwasi kwa wanakijiji wa Kanyaga. Baaadhi ya wakazi wa vijiji vya jirani walikuja kuomba hifadhi au makazi ya kudumu katika kijiji cha Kanyaga kwa sababu ya chuki na uhasama wa wao kwa wao au na viongozi wao. Wanakijiji hata wa vijiji vya jirani walimwamini na kumpenda sana Ntemi wao Dongwe.
Dongwe alikuwa masikioni, midomoni na mioyoni mwa wanakijiji wote. Lilikuwa sio jambo la kushagaza kuona raia wakienda Ikulu, nyumabani kwa Ntemi kupeleka shina la muhogo lililozaa isivyokawaida au kondoo, mbuzi au ng’ombe aliyezaa mapacha alikuwa yeye na ndama wake ni mali ya Ntemi. Na watu walikuwa wakienda kufanya matambiko kwenye miungu yao ya familia kwa ajili ya mifugo yao kuzaa mapacha ili waipeleke kwa Ntemi. Ilikuwa ni sifa kwa kijiji kizima kupeleka kitu kilichotofauti na vingine kwa Ntemi.
Kwa bahati mbaya Ntemi alipofikisha umri wa miaka 20 akaanza kuugua maradhi yasiyojulikana. Akaitwa mganga mkuu anayeaminiwa na kijiji kizima ili aweze kuokoa maisha ya Ntemi huyu aliyependwa na kijiji kizima. Wanakijiji wakawa wakimuombea Ntemi wao kwa miungu yao ili aweze pata nafuu na kuwaongoza kama ilivyokuwa kwa miaka yake iliyopita. Mganga tegemeo la kijiji kizima baada ya matibabu ya mlima wa mizizi kuonekana kutofua dafu akatangaza kushindwa.
Basi watu wakawa wakijaribu kila dawa waliyoiota labda ingempa mfalme Amani lakini haikuwa hivyo. Ntemi alikuwa akinukia shubiri wakati mmoja na wakati mwingine angenukia mdalasini, iriki na karafuu lakini bila nafuu. Wakawatangazia wanakijiji wa vijiji jirani nao kwa upendo na Ntemi huyu walikuja na mizizi ya meno, mikaa ya migomba na nini sijui lakini hali ya mfalme ikawa mbaya Zaidi. Waganga wakatoa tofauti zao wakakaa kikao kwa ajili ya kumuokoa mfalme lakini bila mafanikio.
Dau likatangazwa kwa vijiji vya mbali Zaidi kama kawaida ya waganga wakatandika punda wao wakawabebesha mizigo ya mizizi, mafuvu ya fisi na vyote wanavyovijua waganga. Lakini mfalme hakutoa hata jasho la ahueni. Watu wakakata tamaa wakaweka dawa zao pembeni na kuanza kufanya usihiri kuzungunga ikulu lakini wapi nafuu ya Ntemi?!
Habari za kuugua kwa mfalme zikayafikia masikio ya Marando, japo alikuwa mzee wa umri lakini hakuwahi kusahau kuwa moyo wake ulifurahi kuishi katika kijiji cha Kanyaga. Marando alikuwa na binti aliyeitwa Maua, Maua alikuuwa maua kweli mrembo sana mwenye umri wa miaka 18 hivi. Aliposikia ugonjwa wa Ntemi akampasha habari binti yake kuwa wakati wa kurudi kuishi katika kijiji cha Kanyaga kwa furaha na Amani umewadia. Maua alihamaki wangerudije na wakati walitakiwa kuuwawa?
Marando akamwambia dawa ya mfalme ninayo mimi na sitavumilia kuona Ntemi mwenye moyo mzuri kama yule anapoteza maisha. Maua akakubaliana na baba yake na kwenda Kijijini Kanyaga. Kwa sababu watu walikuwa wamekwisha wasahau hivyo hata hawakutaka kwenda kwa kujificha walienda mchana kweupee. Waliposema wana dawa ya kumtibu mfalme basi wakapewa walinzi kuwasindikiza kwenda kwa mfalme. Moja kati ya walinzi wale alikuwepo Mtupa rafiki kipenzi wa Marando. Marando alimtambua ila hakumwambia neno lolote.
Walifika kwa Ntemi na kabla ya matibabu kuanza, Marando alimuuliza Ntemi kwa sauti ya kinyenyekevu kuwa alikuwa anaumwa nini. Walinzi wakamwambia Marando, ‘‘Mganga hilo swali bwana Ntemi huwa hapendwi kuulizwa, we mtibu tu kama una dawa kweli atapona atapona.’’ Maranda akawahakikishia kuwa dawa yake ipo kwenye maongezi na kwamba kama mfalme angeongea tu yeye dawa yake ingeanza kazi.
Siku ya kwanza ilipita mfalme hakuongea neno. Alikuwa anajigeuza tu huku na kule na kuguna kana kwamba ana maumivu makali sana. Alikuwa akikaa muda anashusha pumzi kwa nguvu kama mtu anaetaka kata roho. Siku sita mganga huyu alikuwa tu chumbani mule kwa Ntemi akisubiri kusikia sauti ya Ntemi. Waganga wengine Ntemi alikuwa anawaoneshea ishara ya kuwafukuza pale tu walipomtaka aongee lakini haikuwa hivi kwa mganga Marando na binti yake Maua. Kadiri walivyozidi kukaa ndivyo mfalme alivyokuwa akijisikia Amani na kula chakula chake vizuri kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Walinzi walikuwa wakishangaa kumuona mganga huyu ambaye hakuharibu msitu kwa kuleta tela la mitishamba kama wenzake. Wakawa wakisemezana kuwa kweli duniani kuna waganga yani anataka Ntemi amjibu tu ili aanze kupona. Hili nalo linaweza kuwa mfano wa ajabu la dunia. Wabeba mikoba, wazee na wanakijiji walihamaki kusikia kile kinachoendelea kwa Ntemi. Wote wakatamani kumshurutisha Ntemi aongee lakini Mganga na binti yake waliwaambia kutokumshurutisha maana wangeharibu dawa yake.
Tatizo la siku na wiki ni kama una kitu unachosubiria kwa hamasa sana huwa zinaenda polepole mwendo wa konokono. Watu walikuwa wanaona kesho za jana zikipishana kwa kasi ya kinyonga bila Ntemi kuongea na mganga wao. Lakini hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, siku moja baada ya chakula cha mchana mfalme akawafukuza watu wote toka chumbani. Watu wakatoka kwa furaha wakijua kuwa Ntemi wao amechagua kupona siku ile. Watu wakaenda kusimulia kila kilichokuwa na masikio na taarifa yao ilikuwa na wasikilizaji wengi mno.
Mfalme akamwambia Marando, ‘‘mimi sijui naumwa nini! Ila nilipowaona nyinyi nimeanza kupata nafuu.
‘‘Huwezi kuwa hauumwi kitu mtukufu Ntemi, kuna kitu kinakudhoofisha’’ alijibu Marando.
‘‘Kiukweli nilianza tu kujisikia moyo unakuwa mzito mpaka nashindwa kufanya kazi zangu.’’ Ntemi alijaribu kujieleza.
Baada ya udadisi mkubwa Marando akamwambia Ntemi kuwa ameugundua ugonjwa wake na siku iliyokuwa inafuata wangeenda kuchimba dawa wakiwa watatu tu. Hawakutaka mtu mwingine awafuate maana wangeenda kuharibu dawa ya Ntemi. Watu walikubali na Ntemi pia alikubaliana na ombi lile.
Mara baada ya kifungua kinywa asubuhi iliyofuata basi Ntemi, Marando na Maua wakaongozana kuelekea msituni, Ntemi akiwa katikati na Marando akiongoza njia huku Maua akiwa nyuma na amebeba jembe mkononi mwake. Walitembea kimya kimya wakimtaka Ntemi azidi kutafakari kuhusiana na kitu chochote kinachomsumbua ili wamchimbie dawa huko waendako. Walipofika njia panda ya kwenda msitu wa tambiko na ile inayoenda kijijini kwa Marando wakasimama.
Mara Marando akamgeukia mfalme na kumwambia mfalme akumbuke kuna kitu alilowahi kukifanya njia panda. Mfalme akamwomba iwe siri kwa sababu ni siri aliyoitunza maisha yake yote. Ntemi akasema nakumbuka baba yangu alitoa amri kwa msichana kashindye aliyekuwa na wiki moja tu kuja kutupwa msitu wa tambiko lakini mimi niliwafuatilia nyuma wale wauaji na kumchukua motto pale walipokuwa wamemuweka ili ajifie au aliwe na wanyama wakali.
Baada ya kumchukua mototo yule Ntemi hakujua ampeleke wapi mara kwa nasibu akapita mwanaume wa makamu akielekea kijiji cha mbali kwa njia inayoelekea kijijini kwenu. Ntemi akamuomba yule mwanaume aende kumtunza yule binti na akikua ajitahidi kumleta japo amuone tu kwa siri. Basi yule mwanaume alikuwa mkarimu sana na kuniambia angefanya vile alivyoombwa na Ntemi Dongwe. Lakini miaka imepita mingi bila Ntemi kusikia taarifa ya yule binti hivyo alidhani huenda aliukabidhi mzimu na ulienda kumdhuru yule binti.
Ntemi akasimulia namna ambavyo Marando, kashindye wa kwanza alivyoenda kuchinjwa bila huruma katika msitu wa tambiko. Huzuni ile aliapa kutoiruhusu itokee tena maishani mwake na ndio maana alipoona wanaenda kumtupa yule binti wa wiki moja alipanga kumsaidia licha ya kwamba hakujua angempeleka wapi. Basi, mfalme akawa muwazi kwa mganga huyu asiyemfahamu na kumuomba asitoe ile siri yake ya kuugua ugonjwa usiojulikana.
Marando na Maua wakajikuta wakibubujikwa na machozi na kuangua vilio kwa pamoja. Ntemi akahamaki sana na kuuliza kulikoni. Marando akamsimulia kwanza mkasa wake na jinsi vijana Mtupa, Sangijo na Kitinde walivyoyanusuru maisha yake na pili akamkumbusha kuwa yeye ndiye aliyemchukua Maua na kwenda kumlea mpaka alipokua. Marando baada ya kusaidiwa aliamua kuja kulipa fadhira kwa Maua ambaye alipata taarifa zake kwa wachota maji wa kijiji chake kuwa angetupwa porini na akaamua kuja kumuokoa. Marando akasema nilijua kama kweli Ntemi angekuwa anakumbuka fadhira zake mawazo yake yasingemtulia. Ndiyo sababu hakuleta taarifa yoyote ya Maua kwa Ntemi.
Ntemi alifurahi sana na kuwaamuru kuwa ile siri iwe miongoni mwao tu. Waliporudi kijijini Ntemi akawashangaza Marando na Maua baada ya kutangaza kuwa wiki inayofuata alikuwa anaoa na angemuoa Maua kwani ndiyo dawa yake. Kwa hiyo watu wakaadhaa sherehe ya harusi ya Ntemi. Watu walikula, walikunywa na walicheza kwa wiki nzima. Kashindye akawa malkia pasipo na mtu yeyeto kung’amua.

HADITHI YA 4: MAGANGA CHA POMBE
Maganga ni kijana wa makamu alieishi upande wa magharibi wa kijiji cha Kanyaga. Maganga licha ya kuwa kijana mdogo aliyekuwa anakadiriwa kuwa na umri wa miaka kama selathini hivi, alikuwa tayari ameshaoa mitala ya wanawake watano, huku akiwa na mtoto mmoja. Mke mkubwa wa Maganga alijulikana kwa jina la Kabula au mama Wande. Mke wa pili aliitwa Nchoji, mke wa tatu aliitwa Milembe, wanne aliitwa Siha na watano aliitwa Masele.
Maganga alikuwa kijana mchapa kazi sana aliyeyejishughulisha na kilimo cha mpunga, mahindi na miwa. Kila mwaka alikuwa na uhakika wa kuvuna magunia mia na hamsini ya mpunga na magunia mia na ishirini ya mahindi. Kabla hajaoa alikuwa akiuza mazao yake siku ya gulio na kununua ng’ombe ambao walimsaidia Zaidi kwenye shughuli za kilimo. Kuna kipindi aliwahi fikisha jozi kumi na nane za Nzagamba, maksai wa kulimia.
Wazazi wengi walikuwa wakimpigia mfano kijana Maganga kwa vijana wao wavivu na wasiojishughulisha. Kwa wazazi wengi walitamani sana vijana wao wawe kama Maganga. Maganga hakujua kwenda kukaa kijiweni kula miwa na kupiga soga kama vijana wengi wa kijijini pale walivyofanya. Yeye aliamka kabla ya mawio ya jua na kuelekea shambani au kwenye majaruba yake ya mpunga kwa ajili ya kulima, kupalilia au kuangalia maendeleo ya mazao yake.
Kusema ukweli Maganga alikuwa ameliteka hata soko la mazao kijijini pale. Maana yeye alikuwa akiweka akiba ya mazao yake stoo na kusubiri yakiadimika ndipo aanze kubadilishana na mifugo. Msimu wa kuvuna mazao ulipofika Maganga ndiye alikuwa mnunuzi mkuu wa mazao ya wanakijiji wengine. Na wanakijiji walipenda kumuuzia mazao kwa kuwa hakuwafanyia dhuruma bali aliwalipa kwa kiwango walichokitaka au kukubaliana.
Shida huwa hazipigi hodi, hivyo Maganga alikubali kufuatwa hata usiku wa manane kwa ajili ya kufanya biashara au makubaliano ya kibiashara. Wakati mmoja alipokuwa hajaoa bado dada mmoja alikuja kugonga mlangoni kwa Maganga usiku wa giza totoro. Maganga akauliza akiwa ndani kuwa ni nani aliyekuwa akigonga mlangoni. Sauti ya kike nyororo ilijibu kuwa, ‘‘Ni mimi Kabula.’’ Maganga akafungua mlango na kumsikiliza mgeni wake akiwa mlangoni bila ya kumkaribisha ndani.
Kabula alikuwa amekuja kuomba msaada wa tela la ng’ombe linaloendeshwa na jozi moja ya ngombe ili ampeleke baba yake kwa mganga wa jadi maana alikuwa hoi bin taabani. Kabula akamwambia alijitahidi kwenda kumuita mganga aje amtibu baba yake nyumbani kama ilivyokuwa utaratibu wake lakini alimkuta akiwahudumia wangojwa wengine pale kwake na isingekuwa rahisi kuwatelekeza bila msaada. Hivyo basi Maganga alimsaidia Kabula kufunga jozi moja ya Nzagamba. Maganga pia alimsaidia Kabula kwenda kumpakia na kumshusha baba yake kwenye tela maana nyumbani kwa kina Kabula hawakuwa na kijana wa kiume.
Baada ya siku mbili kupita Kabula alikuja nyumbani kwa Maganga lakini hakumkuta. Alipowauliza majirani wakamwambia aliwaaga kwenda kuangalia shamba lake la miwa ambalo halikuwa mbali. Dada wa watu akamfungia safari na kumfuata mpaka shamba la miwa la Maganga. Kwa nasibu alimkuta akiwa anafyeka majani yaliyoota katika njia ya kuliingia shamba lake.
Kabula alisalimia kwa heshima ijapokuwa kiumri alimzidi Maganga miaka kama mitano hivi. Lakini mila na desturi za Kanyaga, mwanaume alikuwa anazaliwa akiwa mkubwa tayari. Hata mama yake Maganga humweshimu Maganga kama baba yake, na hata alimpa jina la babu yake kwa heshima. Kabula alikuwa amekuja kukopa mbuzi wawili ili aende akamlipe mganga aliyeyaokoa maisha ya baba yake.
Kabula alikuwa ni mpishi wa pombe maarufu pale kijijini lakini kipindi cha masika wateja wake walikuwa wakinywa kwa mkopo wa kuja kulipa baada ya mavuno. Hivyo hakuwa na kitu chochote cha kumlipa mganga wake wa jadi na kama ilivyojulikana pale kijijini mizimu huwa haikopwi tiba. Maganga alimwelewa na kumsaidia kuwapata beberu wawili kama malipo ya mganga wa jadi. Kabula alilengwa lengwa na machozi ya furaha na kumuaga Maganga huku amepiga magoti ya heshima.
Maganga alibaki peke yake ndani akimuwaza Kabula kinagaubaga. Alijikuta akimuumba upya Kabula binti Masanja. Kiukweli alikuwa ni msichana mlimbwende sana, mwenye heshima na ustaarabu wa hali ya juu. Vijana wengi pale kijijini walimuogopa kwa sababu alikuwa hapendi mizaha ya hovyo hovyo. Maganga alijikuta anampenda Kabula ila alikuwa hawezi kuongea na msichana yeyote kuhusu mapenzi na ndoa. Mawazo ya Kabula yakamletea usingizi mzito na akalala kama pono.
Alishitushwa toka usingizini na hodi za mfululizo zilizogongwa mlangoni. Kwenda kufungua mlango akabaha alipokutana na uso wa mviringo wa Kabula. Akamkaribisha ndani huku akimpokea kikombe kikubwa kilichokuwa kimefunikwa. Alipoingia ndani, Kabula akaomba radhi kwa kumuamsha Maganga toka usingizini. Akamwambia moyo ulimsukuma amletee pombe yake kidogo ili aonje. Maganga alikuwa sio mnywaji wa pombe. Hata kwenye sherehe kubwa alikuwa akitumia togwa tu.
Lakini zawadi inanguvu ya kubadili maamuzi na mipango ya mtu ya muda mrefu. Wakati Maganga akiwaza labda amsubiri Kabula aondoke ili akaimwage pombe yake, mvua kubwa ikaanza kunya kijijini Kanyaga. Kwa sababu Kabula na Maganga walikuwa hawana mazoea wakajikuta wakikosa cha kuongea. Kabula akachukua kile kikombe cha pombe na kukikabidhi kwa Maganga kwa magoti ya heshima huku akimwambia, ‘‘Karibu uonje pishi langu sijakuwekea kilevi sana maana najua huwa hupendi pombe.’’
Yale magoti na ile sauti nyororo vilifanikiwa kumtoa nyoka pangoni. Kijana Maganga akapokea kile kikombe akakata mafundo mawili ya uhakika kikombe kikabaki nusu- nusu ya kujaa au nusu tupu vyote sawa ila inategemeana unamuwazia nini Kabula. Baada ya kupita dakika kama tano za ukimya, ukimya mzito wa kukata na shoka, Maganga akaanza kupayuka kwa sauti ya juu. ‘‘Wewe, Kabula ni mzuri sana. Mimi nataka nikuoe sasa hivi.’’ Maganga akamalizia mafundo yake mawili na akamsogelea Kabula.
Baada ya mvua kuisha nao wakawa wamekwisha kabisa na Kabula akaaga kwa heshima na kuondoka. Ulevi ulikuwa haujamuisha Maganga na Kabula alijua fika ila akaondoka. Lakini ondoka yake ilikuwa ondoka ya kurudi tena kwa sababu alifunga mlango kwa nje. Kiza kinene kilitanda na Maganga akiwa anajiongelesha tu mule ndani kwake. Mara mlango ukafunguliwa, Kabula akaingia akiwa na kapu la chakula. Maganga akampalamia Kabula lakini Kabula alikuwa mpole na mwenyekusihi sana kwamba wale chakula kwanza, hivyo Maganga akakubali kula chakula cha kwenye kapu halafu waangalie uwezekano wa chakula kilichodondokea chini ya sketi.
Hivyo ndivyo Kabula alivyoolewa na Maganga au tunaweza kusema, Kabula alivyojioza kwa Maganga. Maganga akaanaza kuwa mlevi mzuri wa pombe ya mke wake. Alikuwa anakunywa mara moja kwa siku, akajikuta anaongeza idadi kuwa mbili, tatu mpaka akawa hawezi ishi kwa lisaa limoja bila ya kunywa pombe. Kabula alimkaa haswa moyoni na pombe ikapata nafasi yake kichwani. Pombe ikawa ndio kazi na kazi ikawa ndio pombe. Kuna siku alikunywa pombe mpaka akajinyea uharo palepale alipoketi.
Mapenzi huleta watoto kama mizimu ya ugumba haijamkasirikia mwanamke ndivyo ilivyoaminika pote katika kijiji cha Kanyaga. Kabula akawa mjamzito. Na kwa bahati mbaya mimba yake ikamwendesha kweli kweli. Akawa hali chakula maana akila tu anatapika mpaka nyongo. Akawa hafanyi kazi yoyote isipokuwa kulala na kula udongo, ndimu na maembe machanga. Mlevi aliyepindukia, Maganga akajikuta katika wakati mgumu sana. Kuishi bila pombe ilikuwa ni mwiko kwake, akaanza kuitafuta pombe vijiji vya jirani.
Ulevi wa Maganga ulikuwa mbaya sana, japo sijawahi kuona ulio mzuri, kwani baada ya kichwa chake kulewa mikono yake ilitaka papasa sehemu za miili ya wanawake waliokuwepo kirabuni pale. Kuna siku alilewa chakali halafu akaanza kumtomasa mwanamke aliyekuwa karibu nae.  Lilikuwa kosa la jinai maana mumewe alikuwa nae pale pale kirabuni. Maganga alipigwa vichwa vya mdomo, makofi na mitama mpaka watu wakamuonea huruma na kumuokoa. Akarudi nyumbani akiwa amelowana damu kwenye nguo zake zote na uso wake ulivimba sana hasa maeneo ya mdomoni. Mke wake alipomuona alilia sana. Maganga aliogeshwa, akakandwa na kubadilishwa nguo.
Asubuhi yake pombe zilipomtoka alijuta sana akaapa kwa mzimu wa baba yake kuwa asingelewa tena. Lakini mlevi ni mlevi tu hata kitokee nini. Matukio huwa hayambadilishi mlevi labda aishiwe kiu ya ulevi wake. Zilipoisha siku mbili, Maganga akapata hamu ya pombe hadi kichwa kikaanza kumuuma. Akawaza na kupata sulihisho kuwa angeenda kijiji kingine na hata kuwa mgomvi tena. Baada ya kujishauri akaondoka nyumbani bila kuaga akaenda kijiji kingine kutafuta pombe. Alipofika kule akaanza kujitapa juu ya mafanikio yake. Na wengi wao walikuwa wakimfahamu vizuri.
Baada kuwa wamekunywa mpaka karibia usiku wa manane, mzee mmoja alimkaribisha kwake ili apumzike kwa usiku ule. Maganga alikubali wito kumfuata mzee yule mpaka nyumbani kwake. Mwenyeji wake alimuonesha chumba cha kulala na kumuwashia kibatari. Maganga aliletewa chakula na binti wa pale nyumbani. Binti alikuwa mlimbwende hasa, matatizo akawa anameza tu funda baada ya funda la mate. Alikula chakula huku binti amepiga magoti pembeni yake. Uzalendo ukamshinda, akamuuliza jina lake ambalo hakuwa hata na kazi nalo. Binti alimwambia kuwa aliitwa Nchoji.
Maganga aliacha kula na kuanza kukichungunguza kifua cha Nchoji. Kipimo cha uvumilivu kilikuwa kimefika kikomo kwa Maganga. Akasimama akaenda funga mlango halafu akamwambia, binti nataka uwe mke wangu. Twende wote Kanyaga tukale mali zangu maana ni nyingi mno siwezi zimaliza peke yangu. Ila ninaombi moja tu, ukinikubalia tunaenda wote Kanyaga. Ombi lenyewe hata halikuwa ombi bali lilikuwa takwa maana Nchoji alikuwa hajaelewa bado nini kikiendelea mlevi akawa ameshafika kifuani na baada ya muda akamlaza kwenye ngozi iliyokaribu nae na kujikaribisha kwa huduma, ambayo muombaji alikuwa hajakubali wala kukataa.
Nchoji alishindwa kupiga kelele licha ya maumivu aliyokuwa akiyapata. Hakujua kwa nini ila umasikini wa nyumbani kwao ulichangia yeye kukaa kimya ili kwa machungu haya ya muda aende kufurahia maisha huko Kanyaga. Asingeweza kukimbia maana baada ya yote alitakiwa alale na mgeni japo kwenye ngozi tofauti. Wakati mawazo yakimzunguka kichwani Nchoji, mlevi alishuka na kulala pembeni yake huku akimtomasa tomasa sehemu zake za kifuani.
Asubuhi mzee mwenye mji na Maganga walipangiana mahali ya ng’ombe ishirini na wangeenda kuchagua wenyewe kwenye zizi la Maganga kijijini Kanyaga. Msafara ulijiandaa, Nchoji hakuwa na vitu vingi vya kubeba sana sana alijibeba mwenyewe tu, mama yake alipiga vigeregere vya furaha na vya kumuaga binti yake. Wanakijiji walisemezana kuwa Nchoji ameukata. Amewaachia shida zao pale kijijini kwao. Msafara uliongozwa na mwenyeji Maganga na kufuatiwa na Nchoji, Baba yake Nchoji, Mjomba wake Nchoji na walevi wawili. Safari ilikuwa ndefu lakini walifika na kumkuta Kabula kajilaza hoi kwenye kivuli cha mwembe ulio karibu na nyumba.
Maganga alimuita mkewe pembeni na kumwambia kuwa amemletea msaidizi pale nyumbani. Japokuwa Kabula hakupenda kuolewa mke mwenza mapema vile ila aliufyata mkia. Nchoji akakabidhiwa jiko, vijana wakachinja mbuzi na sherehe ndogo ikafanywa na baadae baba mkwe akabagua ng’ombe wake toka zizini na kuanza safari ya kurudi kijijini kwake. Nchoji alipewa chumba chake cha kujitegemea na Maganga akawa akilala au kujipumzisha kwenye chumba cha Nchoji tu. Wivu ulimshika Kabula lakini hakuwa na uwezo wa kufanya chochote.
Maganga alioa wanawake watatu wengine kwa mtindo huu huu kama alioutumia kwa Nchoji. Alipoenda kulewa tena mzee mmoja alikuwa akimchangamkia na kumywesha pombe nyingi na baadae kumkaribisha nyumbani. Wake walioongeza ukubwa wa familia ya bwana Maganga ni Milembe, Siha na Masele. Wake walioolewa baada ya Kabula wote walikuwa wadogo wadogo wenye umri kati ya miaka kumi na tatu hadi kumi na saba. Hivyo wote walizidiwa kiumri na Kabula mbali sana.
Siku moja Kabula akawashauri wake wenza waanze kupika pombe pale kwao maana mume wao angeoa kijiji kizima kwa tabia yake. Wakafanikiwa kumdhibiti kwa pombe maana kila akikohoa aliletewa pombe na moja kati ya wake zake. Aliona maisha yamemnyookea maana aliiishi kama mfalme pale nyumbani. Alikuwa kiletewa vyakula muda wote mpaka vingine akawa akionja tonge mbili ili kumfurahisha mke wake aliyeleta chakula kwa zamu yake.
Mbinu ya wake zake na Maganga ilizaa matunda kwani ilipita miezi sita bila mume wao kuongeza mke mwingine au kwenda kulewa kijiji cha jirani. Kwa bahati mbaya sana mbinu yao iliishiwa nguvu mara pale wote walipojigundua ni wajawazito. Kila mmoja akawa akitafuta udogo, ndimu au ukwaju ili kuondoa kichefuchefu mdomoni mwake. Maganga akawa huru tena kutembelea virabu vya pombe vya vijiji vya jirani.
Siku moja baada ya kunywa na kulewa haswa hadi akalala na kutoa haja ndogo na kubwa pale pale akakosa mfadhili wa kwenda nae nyumbani. Alikuja kuzinduka saa saba za usiku na kuanza safari ya kurejea nyumbani. Kwa bahati mbaya alipofika msituni akajikwaa kwenye kisiki na kuanguka. Alishindwa kuamka kwa sababu ya uchovu aliokuwa nao. Akaazimia alale kidogo akiamka ataendelea na safari. Akalala fofofo.
Kiumbe chatu akiwa kwenye mawindo yake akitafuata kitoweo. Chatu alijiona mwenye ngekewa baada ya kukutana na kitoweo kimejilaza tena kando ya njia. Chatu akaanza kuuramba mwili wa Maganga ili ateleze vizuri kuingia tumboni mwake. Chatu akaupakaza mate mwili mzima wa Maganga. Akaanza kummeza kuanzia miguuni. Kwa nasibu, Maganga alilala huku ametanua msamba. Hivyo chatu aliumeza mguu mmoja tu wa Maganaga na kushindwa kuendelea kwa sababu mguu mwingine ulikuwa mbali, hivyo akatulia.
Maganga fahamu zilipomjia kwenye usingizi wake akajisijia joto kwenye mguu wa kushoto. Akajisemea kimoyomoyo, ‘inamaana leo mama wande ameamua kunifunika mguu mmoja tu.?’’ Basi akaamua kuulazimisha na mguu wa kulia kinywani mwa chatu na kujisokomeza mwili mzima mdomoni mwa chatu. Na chatu hakufanya ajizi, akammeza. Maganga akamezwa na chatu. Ndio maana hadi leo wanakijiji wa Kanyaga hawaendi kunywa pombe vijiji vya jirani.

HADITHI YA 5: MAKOYE, MCHAPA KAZI MWENYE BAHATI YA KIFO         
Zamani za utawala wa Ntemi Doi, kijiji cha Kanyaga kilikuwa kikipigana vita sana na vijiji vya jirani. Vita hizi zilikuwa zikitokana na baadhi ya vijiji kutafuta mateka wa vita ambao wangewatumia kwa ajili ya shughuli za kilimo ili kuongeza uzalishaji kijijini mwao. Vijiji vilivyokuwa vikipenda kuja kwa mapigano ya vita vilikuwa ni kijiji cha Ikindika na kijiji cha Nyahanga.
Siku moja kijiji cha Ikindika kilivizia mnamo usiku wa manane na kuchoma nyumba nyingi za kijiji cha Kanyaga. Wanakijiji wa Kanyaga walikimbia hovyo hovyo na kuuawa kama kuku. Wanaume wenye misuli walichukuliwa pamoja na wanawake walimbwende wa kijiji. Mifugo iliyonona pia yote ilibebwa na maharamia wa kijiji cha Ikindika. Kijiji kilibakia na wazee, watoto na wanawake. Ntemi Doi na walinzi wake walikimbilia porini kujificha.
Moja kati ya vijana waliokamatwa alikuwa ni Makoye. Makoye alikuwa mchapa kazi sana. Alikuwa na ng’ombe wake aliowatenga kwenye makundi mawili kila kundi ng’ombe mia tano. Alikuwa na mbuzi wasio na idadi na kuku aina ya kuchi ambao kila mtu alikuwa akiwatamani pale kijijini. Maharamia wa kijiji cha Ikindika walibeba mali nyingi za kijana Makoye bila kujua. Kweli mali inamfuata mwenye nayo, waliobaki kijijini pale walijisemea.
Njiani kote Makoye alikuwa akiwaza kuhusiana na kupoteza mali zake zote kwa pamoja na pigo baya zaidi ni yeye kuchukuliwa kuwa mtumwa. Makoye alijikokota kuelekea utumwani asikokujua na mbaya zaidi alikuwa amemposa binti mlimbwende wa kijiji kizima, Masele binti mfalme. Sherehe yao ya harusi ilibakiza siku tatu tu ifanyike hata hivyo maandalizi yalikuwa yakifanywa kwa umakini wa juu mno. Hata kabla ya usiku huu wazee walikutana kwa ajili ya kupanga ratiba ya upishi siku ya harusi.
Lakini vita huwa haina macho, yenyewe huharibu mipango ya watu na hata kukatisha maisha yao. Wakati wakitembea kuelekea kijiji cha Ikindika kilichopo umbali wa maili kumi na nane hivi toka Kanyaga, jua lilianza kuchomoza hivyo watu wakaanza kutambuana kwa sura. Makoye kutupa jicho huku na kule akamuona kipenzi chake Masele binti mfalme ameshikiliwa mkono na ambaye alikuwa kiongozi wa jeshi la jadi la Ikindika. Alitamani kutabasamu lakini hakuweza kwani kipenzi cha moyo wake naye alikuwa ametaifishwa.
Baada ya safari ndefu huku Makoye akitamani kufa kuliko kuendelea kuyaona anayoyaona, aliamua kujiangusha chini makusudi. Walinzi wakatumwa kumuamsha, akajilegeza kweli kweli ili wamuache au wamuue. Maana ilikuwa inasemekana jeshi la jadi la ikindika likiwateka wanyonge na waliochoka walikuwa wakiuawa au kuachwa wajifie kwa njaa na uchovu. Lakini haikuwa hivyo kwa Makoye, kamanda wa jeshi aliamuru apewe maji na chakula maana alisema huyo angeenda kufanya kasi kwa mfalme wao.
Maneno yake yalimtia nguvu kidogo Makoye lakini alitamani amuombee na Masele binti Ntemi aende nae kwa mfalme, lakini alikuwa mateka na huenda mazungumzo zaidi yangesababisha kugundua mahusiano yao na mbinu zake. Hivyo alikaa kimyaa kama hajui chochote. Safari ilikuwa inaonesha matumaini kwani waliona nyumba zilizokuwa bondeni baada ya kuukwea mlima Ikindika. Matumaini yakarejea japo hawakujua maisha ya mateso yao yangekuwaje.
Walifikishwa kwenye ua wa mfalme na mfalme wao akaanza kuchagua watumishi wake. Wakwanza kuchaguliwa alikuwa Makoye, na wanajeshi wa jadi wakapiga makofi ya kushangilia maana ndilo lililokuwa chaguo lao hata kabla mfalme hajachagua. Alimchagua na mfungwa mwingine wa kike lakini hakuwa Masele maana mfalme alikuwa hataki mabinti weusi hivyo Kidiga, binti mweupe akajizolea sifa ya kuwa mke mdogo wa mfalme.
Wanajeshi wa jadi pia walijichagulia wafanyakazi wa mashambani na wanawake wa kuoa. Masele akaangukia mikononi mwa kamanda wa jeshi. Makoye alitamani kulia ila akajikaza, alipomuangalia Masele pia alikuwa akilia maana alikuwa anampenda sana Makoye. Watumwa waliobaki walipigwa mnada kwa waliokuwa na uwezo na mali ikatunzwa kwa mfalme. Watumwa wapya walipata tabu sana kwa sababu kila aliyenunua mtumwa alitaka kurudisha gharama ndani ya muda mfupi.
Lakini haikuwa hivyo kwa Makoye, yeye alipewa uhuru wote wa kufanya kazi kwa moyo wake ili kumuongezea mfalme utajiri. Haikupita muda Makoye alipewa kuwa msimamizi wa watumwa wenzake pale kwenye utawala wa Mfalme wa Ikindika. Akawa akiwaongoza kwa upendo na furaha hivyo kila mtumwa alimpenda sana Makoye. Hata watumwa waliochukuliwa toka vijiji tofauti na Kanyaga walikuwa wakimpenda sana Makoye. Msimu wa mavuno ulipofika mazao ya mfalme yalikuwa mengi na bora kuliko watu wengine. Makoye akasimamia utunzwaji wa mazao stoo kwa mpangilio uliomfurahisha sana mfalme. Mfalme akamuongezea wajibu wa kusimamia mifugo yake pia iliyokuwa ikichungwa na kufugwa kwenye pori la jirani.
Makoye alifanya kazi kana kwamba anafanya kazi yake. Maziwa ya ng’ombe yakawa hayakatiki Ikulu. Watu walikunywa maziwa mpaka wakashangaa. Hata wafanyakazi wa chini walikuwa wakibeba maziwa walipokuwa wakirudi majumbani kwao. Makoye aligundua kuwa wachungaji wa mifugo walikuwa wavivu wa kukamua na waliyokuwa wakikamua walikuwa wakibadilishana na chakula toka kijiji cha jirani. Hakuwachongea kwa mfalme ila aliwataka kufanya kazi kwa juhudi zaidi na walimtii.
Masele binti Ntemi yeye alikuwa na hoja zake kule nyumbani kwa kamanda. Maana siku alipopelekwa nyumbani kwa kamanda ambapo alikuwa na wake zaidi ya sita na kila mmoja alikuwa na kanyumba kake. Hivyo Masele akaingia kwenye nyumba aliyokuwa analala kamanda. Kilikuwa ni kijumba kidogo sana kwa nje ila kwa ndani kilikuwa kizuri chenye michoro ya chokaa nyeupe, ya chungwa na nyeupe ukutani. Kulikuwa na kitanda cha kamba chenye ngozi mbili laini juu yake.
Kamanda akamwamuru Masele kwenda kuoga huku yeye akitumia dawa za kienyeji za kuondoa mikosi na mabalaa ambayo vijiji alivyovivamia vingemuombea. Binti Ntemi alirudi akitetema maana alijua lengo la kamanda yule. Wakati akioga alitamani atoroke lakini wanawake na vijana walikuwa wengi hivyo jaribio lake lisingezaa matunda. Akaingia ndani kwa hofu. Alishangaa kuona kuwa kamanda akimuonesha chakula na kuondoka.
Kamanda alijaribu jaribio lake la kumuingilia kimwili binti Ntemi lakini bila kuzaa matunda. Alijaribu kwenda kujaribu kwa wake zake na alikuwa akifanikiwa kuwagaragaza haswa ila alikuwa akimsogelea binti mfalme tu mawazo yake yanamuhama. Siku uvumilivu ukamshinda akamuuliza Masele mbona yuko vile alivyo. Masele akamwambia kuwa alikuwa amezindikwa na mizimu ya babu zake na mwanaume ambaya angejilazimisha tofauti na inavyomwambia nafsi yake basi angekufa. Mwanaume ambaye hata mizimu ilimkubali ni Makoye tu. Kamanda aliogopa sana na kumpeleka kwa Makoye.
Mfalme alimwandalia sherehe kubwa sana Makoye ili amuoe chaguo la moyo wake, Masele binti Ntemi. Watu walifurahi kuona kiongozi wao muelewa na asiyewapa majukumu yaliyowazidi akifunga pingu za maisha. Watumwa walifurahi utafikiri ilikuwa sherehe yao ya uhuru. Makoye akajipatia jiko tena palepale Ikulu. watu walikula, walikunywa na kucheza ngoma hasa.
Baada ya sherehe ya harusi ya Makoye, mfalme alimfanya kuwa kiongozi kwenye serikali ya kijiji chake. Kila mtu kijijini alimfahamu Makoye na aliona kama mfalme amechelewesha uteuzi ule. Watu wote walisaidiana naye katika uongozi vizuri. Ila alikuwa na ombi moja tu kwa mfalme endapo kungekuwa na mpango wa kukiteka kijiji cha Kanyaga basi asihusishwe maana angejisikia hatia kubwa sana. Mfalme alimuelewa na maisha yalikwenda vyema kuliko hata mfalme alivyokusudia.
Mafanikio ya kijiji cha Ikindika yalikuwa makubwa mno kuliko ilivyokuwa hapo awali. Kila mtu akajua mchapa kazi Makoye ndiye chanzo cha mafanikio yale yote. Baadaya kikao cha tathmini ya mafanikio na dira ya kijiji kukaa, mfalme aliamua kumtangaza Makoye kuwa ni Kiongozi wa pili katika utawala wake. Masele binti Ntemi alipigwa butwaa kuona kuwa mumewe alipanda vyeo kiurahisi na bila kipingamizi toka kwa kijiji cha ugeni.
Mfalme akaanza kuugua maradhi yasiyojulikana kwa muda mrefu. Wataalamu wa tiba za asili makundi kwa makundi walikuja ili kunusuru afya ya mfalme. Mfalme alikuwa hawezi hata kuzungumza hivyo majukumu yote yakawa yanatolewa na Makoye na watu walimwamini kweli. Baadhi ya wafungwa wa kijiji cha Kanyaga waliomba ruhusa ya kurudi nyumbani kwani walikuwa wamechoka kukaa utumwani. Makoye akatengeneza sharia nzuri ya kuwaachia huru watumwa wote maana kwa namna walivyoishi kwa raha hata wangeondoka wangerudi wenyewe tu.
Wazee wa baraza waliona ni wazo jema maana lingewaletea watu wengi zaidi pale kijijini ambao wangeomba kufanya kazi za mashambani na kuchunga mifugo yao. Hivyo waraka ukatolewa wa wafungwa wote kuwa huru na kufanya kazi kwa maelewano ya ujira. Wafungwa wengi walifurahi kuwa huru na kwa sababu masika yalikuwa hayajaanza basi walirudi vijijini kwao kwa matumaini ya kurudi tena wakati wa msimu wa kilimo.
Watumwa waliotokea Kanyaga waliopanga siku maalumu ya kurudi nyumbani. Wakatuma mjumbe kwenda kumwambia Masele binti Malkia kuwa walikuwa wamepanga waende nyumbani baada ya siku mbili na walimtegemea sana Makoye ili awaongoze njia. Lakini Masele alipomwambia Makoye akawaomba sana waende na wangemkuta siku ambayo wangerudi, maana utawala wote wa kijiji cha Ikindika ulikuwa chini yake na mfalme angekufa yeye ndiye angekuwa mfalme.
Mateka huru wa kijiji cha Kanyaga walisikitika sana kusikia taarifa za kusikitisha kutoka kwa kiongozi wao waliomtegemea kuwa alikuwa akipambania maslahi mapana ya Kanyaga. Basi Masele binti Ntemi akawa kiongozi wa msafara. Safari ilikuwa ndefu na ngumu hasa pale walipokumbuka wamemuacha mchapakzi shujaa wa Kanyaga. Lakini hata usiku uwe mrefu vipi huwa kuna pambazuka. Mateka huru wakaingia kijijini Kanyaga ambapo palifanyika sherehe kubwa sana ya kuwapokea.
Kila familia ilifurahi kukutana na mwanafamilia waliyempoteza kwa muda mrefu sana. Lakini kwa bahati mbaya sana, kulikuwa na wazee wawili ambao walikuwa ni wazazi wa Makoye. Walikuwa na huzuni kubwa sana na walishindindwa kujizuia walipokosa kumuona mtoto wao mpendwa. Walidhani kuwa amefia huko kwenye utawala wa utumwa, hivyo waliangua kilio kikubwa sana. Lakini Masele binti Ntemi aliwatoa hofu wakwe zake na kuwaambia kuwa alikuwa mzima na walikuwa wameshaoana.
Masele binti Ntemi aliwapa na habari njema kuwa mtoto wao amekuwa kiongozi wa pili baada ya mfalme wa utawala wa Ikindika. Na anatarajia kuwa mfalme muda sio mrefu maana mfalme alikuwa akiugua na angefariki muda wowote ule. Wazazi wake Makoye hawakufurahishwa na uamuzi wa mtoto wao wa kuongoza katika serikali adui na dharimu kwa kijiji chao. Hivyo walilipanga safari ya kwenda kumfuata. Kwa sababu baba yake na Makoye alikuwa mzee sana alibaki kijijini Kanyaga. Safari ikafungwa na msafara wa watu watatu, Mama yake Makoye, mke wake na mdogo wake makoye.
Safari huwa inakuwa karibu kwa anayekufahamu aendako tu, wengine wote hutunza nguvu muda wote. Masele alikuwa anakufahamu kijijini Ikindika ila waliobaki walikuwa wanacheza mchezo wa kubahatisha tu. Walipanda milima, wakavuka mito na mabonde mpaka wakafika katika kijiji cha makatili wasio na haya, Ikindika. Masele aliongoza njia mpaka Ikulu maana alikuwa akifahamika sana. Wazee walishangaa yaani kaondoka jana tu na leo karudi, ama kwa kweli nchi ya Ikindika ilikuwa imebarikiwa.
Makoye aliitwa nje ya Ikulu, alishangaa kumuona mke wake aliyeondoka jana tu. Lakini alipotoka nje na kumuona mama yake machozi yalimlengalenga kwa huruma na furaha kwa wakati mmoja. Mama yake aliyekuwa mnene na mwenye afya njema leo alikuwa amekonda na kuzeeka mno. Akauliza na yule mtu wa tatu alikuwa nani, akaambiwa alikuwa ni mdogo wake aliyemuacha na miaka kumi. Alionekana kuwa kijana wa makamu na mwenye nguvu.
Mama hakupoteza muda akamwambia kijana wake abebe kila kilicho chake warudi nyumbani. Lakini majibu ya Makoye yalimchosha sana mama yake, maana alimwambia alikuwa amemuandalia na kumjengea nyumba ili waje waishi katika nchi ya Ikindika. Mama alijaribu kumkumbusha kuwa watu hawa ndio waliowauwa ndugu zake kipindi cha uvamizi na jeshi la Ntemi mpya, Nchemu lilikuwa linajipanga kulipa kisasi kwa serikali hii ya ikindika. Jitihada zote ziligonga mwamba, akawatawanya kwa kuwaambia kuwa wasubiri angewatumia mtu siku ya kutawazwa kwake.
Mama yake na Makoye hakuamini masikio yake. Alilia chozi la huzuni na kumuaga mtoto wake aliyekuwa akimuwaza kwa miaka kumi na miwili. Walianza safari ya kurudi kijijini Kanyaga wakiwa na maumivu makubwa ya moyo kwani ukitegemea kitu halafu ukakikosa moyo huwa mzito sana. Uzito wa mioyo uliilemea miguu kutembea. Sehemu ambayo walitumia masaa matatu kuja waliyumia masaa nane kurudi. Maana mama alikuwa akifika kwenye jiwe anakaa na kulia sana huku akijiuliza kilimpata nini mtoto wake mpenzi. Chelewa ufike, walifika kijijini Kanyaga mnamo saa nane usiku wakiwa hoi wa miili na roho.
Huku kijijini Ikindika mambo yalionekana kumnyookea Makoye, maana hata kabla mama yake hajafika nyumbani, mfalme akaaga dunia. Moyo wa Matatizo ulikuwa na furaha sana ijapokuwa usoni alionekana kuhuzunika sana. Kwa sababu ilikuwa usiku basi alijitahidi kuitisha vikao vya hapa na pale ili kujua namna mambo ambavyo yangeenda. Hata kama ukifa wenzako wanakula chakula na wanalala kama ilivyokuwa kawaida. Makoye na viongozi wengine walitawanyika kwenda kujipumzisha kwenye nyumba zao.
Alibaki malkia tu na majirani wachache wakilia usiku kucha. Usiku ule Makoye alitamani apate mtu wa kushirikiana nae furaha yake ya kuwa mfalme katika nchi ya ugenini. Alijikuta akikesha tu kitandani na kujigeuza huku na kule kama mlango wenye bawabu mbovu. Mara ghafla kitu kama ndege kikatua juu ya paa lake kwa kishindo. Makoye akalala chali na kuomba awe na macho yanayoona hadi nje. Japo alikuwa sio muoga lakini hakupendwa kushituliwa hasa wakati wa usiku. Wakati mawazo yakitafuta ni nini kilikuwa juu ya paa lake bundi alilia kwa sauti ya huzuni tofauti na milio ile ya kawaida.
Wakati akifikiria zaidi cha kufanya bundi alikuwa akili kwa huzuni. Wazo likamjia kichwani kuwa watu wa Kanyaga wamemtumia bundi ili kumuogopesha arudi nyumbani. Akaamka toka kitandani kwake akachukua upinde wake na mishale akatoka nje. Akamvizia yule bundi wakati bundi analia milio yake ya huzuni Makoye akawa akilenga shabaha yake. Alipomuweka bundi kwenye shabaha akaachia upinde wake. bundi alisikia sauti ya kitu kikivuma akaandaa mabawa yake kuruka, alikuwa amechelewa sana. Mshale wa Makoye ukampata kifuani na kumuangusha upande wa pili wa nyumba.
Makoye akamfuta akauinua upinde wake bundi alikuwa mwisho wa upinde akipambania pumzi yake ya mwisho. Makoye akajisemea moyoni tutaona nani atakaye warudishia taarifa. Akamchukua bundi vile vile kwenye upinde wake akaingia nae ndani. Akakaa kitandani, akawasha kibatari chake akimwagalia bundi yule alipokuwa akikata roho. Bundi alipokata roho tu, akakumbuka mazungumzo ya mama yake, ‘‘huwezi kumgeuza adui yako akupende bila sababu ya msingi, njia nzuri ya kuishi na adui ni kukaa nae mbali.’’ Akazima kibatari chake na kulala usingizi mzito kutokana na kazi nzito alizozifanya mchana kutwa.
Asubuhi ilikucha kama asubuhi nyingine, Makoye aliamka ili aanze shughuli za siku iliyo mbele yake. Akaamka kitandani ili anawe uso maana jua lilikuwa linamchungulia kupitia uwazi wa madirisha yake. Makoye alipoangalia chini akaona mshale wake tu ndo umechoma chini. Ndege wa mabalaa bundi hakuwepo, akaangalia uvunguni mwa kitanda palikuwa patupu. Kuzunguka chumba chake hapakuonesha hata unyoya wa bundi. Akajisemea moyoni mwake kama angeendelea kusumbuka na kumtafuta bundi yule angechelewesha ratiba za mazishi ya mfalme. Hivyo akajipaka maji usoni na kuondoka.
Alipofika nyumbani kwa mfalme akakuta watu wengi wakitikisa vichwa vyao na kumnyooshea vidole. Moyoni akajua kuwa uchifu ameshaupata. Alitaka kuingia ndani lakini walinzi walimzuia wakamwambia kuna kikao cha wazee kilikuwa kikiendelea ndani. Baada ya muda mfupi kiongozi wa wazee alitangaza watu kuelekea sehemu ambapo lilikuwa limechinjwa kaburi la mfalme. Na baada ya mazishi tu angetangazwa mfalme mpya wa Ikindika.
Watu wote walisogea kwenye kaburi, kiongozi wa mila akaingia kaburini na kunyunyizia damu ya ng’ombe kwenye kuta za kaburi na baadae kutoka. Tanganzo la kuushusha mwili wa mfalme kaburini lilitolewa na mwili ukashushwa kaburini. Kabla ya kumfukia, mzee wa mila alitangaza kuwa mfalme huwa anazikwa na mtu wa karibu sana. Mtu aliyekuwa anafanya maamuzi ya serikali hii kwa niaba ya mfalme. Na kuongeza kuwa wazee wote walipendekeza kuwa Makoye ndiye atakayezikwa na mfalme. Makoye alikamatwa kabla hajaongea neno akatumbukizwa kaburini. Vijana wakaanza kumfukia mpaka udongo ulipoisha. Makoye akazikwa akiwa mzima na cheo chake cha usaidizi wa mfalme mkononi.

HADITHI YA 6: LEMI, AJUZA MCHAWI.
Wakati wa utawala wa Ntemi Nchemu Amani na heshima ya kijiji cha Kanyaga ilirudi. Alikuwa amechagua jeshi lake aliloliita Sungusungu. Sungusungu hawakuwa kwa jina bali walikuwa kwa vitendo. Kama ambavyo wadudu sungusungu walivyokuwa wanaweza kushambulia ganda la muwa kwa uhakika na kwa dakika chache tu ganda la muwa lilikuwa likiachwa likiwa kavu kabisa.
Wanakijiji wa Kanyaga walikuwa wakiheshimu msafara wa wadudu walioitwa sungusungu. Kwa sababu wadudu hawa walipotibuliwa msafara wao walikuwa wakimpanda mtu kimya kimya na kuanza kumuuma wakiwa ndani ya nguo tiyari. Hivyo mtu hujikuta akipiga kwata ya bila kuamrishwa na kutamani kuvua nguo zote hata mbele za watu.
Kuna hadithi inapigwa na wazee wa Kanyaga kuwa kuna kijana alienda kutoa mahari ukweni. Sasa kwa heshima na kuwaogopa wakweze akaomba akae sehemu ambayo ilikuwa na ukoka ili awe mbali japo kidogo na wakwe zake. Kwenye ukoka palimwangwa makombo ya wali. Kwa sababu makombo yalikuwa tu, kidogo kijana hata hakuyaona akaketi. Sungu sungu wakampanda kupitia mikononi na miguuni kasha wakaanza kumngata haswa haswa bwana harusi tarajali. Uzalendo ulipomshida alitoa shati na kuanza kukimbia kama mwehu.
Hilo ndilo jeshi la Sungungungu lilivyokuwa likiogopwa na vijiji vyote vilivyokizunguka kijiji cha Kanyaga. Walikuwa wanashambulia bila kuchoka na kwa kupokezana. Wanakijiji wa Kanyaga walijisikia kuwa na uhuru hata wa kuacha mali zao nje kwa sababu sungusungu walikuwa wakizunguka hata usiku wa manane kukagua usalama wa kijiji.
Watu wapenda Amani wa vijiji vya mbali walikuwa wakija kujitafutia hifadhi kijijini hapo. Wazee kwa vijana walikuwa wakionekana kuja na kulowea kijijini Kanyaga. Masharti ya kuhamia hata hayakuwa magumu. Muombaji alipaswa kwenda kwa jeshi la sungusungu na kukaguliwa mali zake zote. Kisha alitakiwa kutumika kwa mwanakijiji mwenyeji kwa mwaka mzima ili ampe eneo lake la kujenga nyumba na kuendesha shughuli zake hapo.
Moja kati ya wahamiaji wa kijijini pale alikuwa Lemi, ajuza. Kwa sababu ya uzee wake sungusungu hata hawakuwa na adhima ya kukagua vifurushi vyake kwani walimuona kutokuwa na madhara yoyote kwa kijiji chao. Watu wa Kanyaga walikuwa na huruma pia basi walimtafutia eneo ajuza Lemi bila ya kumtumikisha kwa kazi za mashambani kwa mwaka mzima.
Ajuza Lemi akawa sehemu ya familia kubwa ya kijiji cha Kanyaga. Mwanzo watu walimshangaa kuona ajuza akijenga nyumba kubwa na nzuri kuliko hata za wananchi waliowengi pale kijijini. Wakadhani kuwa alikuwa na elimu ya uwashi au pengine mumewe, ambaye alisema alikufa miaka mitano iliyopita, alikuwa fundi mwashi.
Siku hazigandi wala kurudi nyuma, huwa zinasonga mbele tu. Ajuza Lemi akawa anakodi mashamba makubwa na kupata mavuno mengi sana. Kuna mwaka alipata magunia mia tatu ya mahindi na magunia mia tatu na kumi na tano ya mpunga. Lakini kilichowashangaza watu wengi, alikuwa hauzi na mwaka mwingine anaingia shambani kulima tena kwa wingi zaidi.
Wanakijiji walipopata shida za chakula ajuza hakusita kuwasaidia tena bila kuhitaji kurudishiwa. Wanakijiji wakampenda sana ajuza akawa ndo kimbilio la wavivu wa kazi pale kijijini. Ajuza akawa akiheshimiwa sana pale kijijini kwa sababu ya roho yake ya ukarimu.
Kuna siku ajuza alikuwa akiulizia mbuzi wa kununua maana anasema alipata ujumbe wa ghafla ndugu zake wangekuja kumtembelea jioni ile. Basi wale waliokuwa wanakula vya bure wakamwambia ajuza apumzike na kwamba wangemsaidia kumletea beberu aliyenona kwa gharama nzuri tu. Kweli juhudi huwa haidanganyi, beberu la miaka mitatu lililokuwa likinuka vumba lilipatikana kwa gharama ya gunia moja tu la mpunga.
Ajuza alifurahi kuona beberu kubwa namna ile kwa gharama iliyokuwa sawa na bure. Wala vya bure wakapima mpunga na kwenda kumkabidhi aliyetoa beberu na kumuhakikishia kuwa wangekuwa pale alfajiri kwa ajili ya kumsaidia kuchinja na kumchuna beberu yule.
Asubuhi waliamka wako hoi sana vijana wale. Walijitahidi kujikongoja ili wawahi kumsaidia ajuza kazi ya uchinjaji na uchunaji wa beberu lake la sherehe. Walishangaa kutokutana na mtu hata mmoja njiani. Watu wa Kanyaga walikuwa wanaamka mapema kila siku hata kipindi cha kiangazi kwa sababu ya shughuli za kulima bustani zao zilizopo mabondeni. Ila leo hawakukutana hata na mwanajeshi mmoja wa sungusungu. Walipiga moyo konde na kuendelea na safari yao.
Walifika nyumbani kwa ajuza ili kumsaidia shughuli waliyokuwa wamemuahidi jioni iliyopita. Walikuwa wamechelewa kidogo tu maana walikuta ajuza anaingiza chungu cha damu ndani. Walipomuangalia beberu alikuwa ameshajichwa na kutundikwa kwenye mti wa mzambarau uliokuwa karibu na nyumba ya ajuza.
Baada ya ajuza kutoka nje tena, vijana wakamuuliza kama angemchuna ngozi yeye mwenyewe. Ajuza aliwaambia hakuhusika na kumchinja yule beberu bali kuna kijana alipita na kumpa msaada tu. Walafi huwa hawachunguzi sana chakula, waliomba visu na kuanza kumchuna yule beberu. Vijana waliona kama alama ya meno ya mnyama mkali kwenye paja la kushoto la beberu yule. Wakati wakishangaa ajuza aliwaambia kuna mbwa alitaka kumla beberu yule baada ya kuchinjwa kwani alikuwa ndani.
Vijana walipewa mabakuli makubwa ya supu ya utumbo na nyama za ndani wakati wakisubiri chakula kiive. Walikunywa supu na kumshukuru ajuza. Walitamani kuaga kuondoka ili warudi nyumbani na baadae wangerudi kwa ajili ya kuonja pishi la wageni lakini haikuwezekana. Usingizi mzito uliwapitia kwenye viti walivyokuwa wamelalia. Ajuza aliingia ndani na kutoka na mkia wa fisi akawagusa wale vijana wawili kwa mkia wake wakageuka kuwa fisi palepale. Akawaswaga wakaingia ndani.
Wazazi wa wale vijana walidhani vijana wao wameenda kumwagilia bustani hivyo hawakuwatafuta. Lakini ilipofika jioni walishangaa kuona vijana hawarudi nyumbani. Walipowauliza rafiki zao, walijibu hawakuwa wamewaona mahali. Walienda kwa ajuza kuwaangalia, maana walijua watakuwa wanakula sherehe kama walivyosimulia jioni yake. Cha ajabu walipofika kwa ajuza hapakuwa hata na dalili ya sherehe au hata harufu ya nyama.
Walishangaa kumuona ajuza akisonga ugali wake na Nsasa, mboga za majani zilizokaushwa. Walipomuuliza kama aliwaona vijana, ajuza akaruka maili mia nane. Alisema yeye mwenyewe alikuwa amempoteza beberu wake. Hivi ndio alikuwa anaingia toka kumtafuta beberu wake na hakumpata. Wazazi wa wale vijana walimpa pole ajuza na kuzidi kuwatafuata vijana wao bila mafanikio.
Watu walidhani kuwa hawa vijana wameraruliwa na wanyama wakali au wamemeza na chatu. Lakini walienda saa ngapi na kufanya nini huko porini, maswali yalikosa majibu. Wazazi wa wale vijana wakaita msiba na watu wakahudhuria kulia msiba usio na mazishi. Kulia bila kuiona maiti nayo inashida zake maana waliaji wengi walishindwa kulia kihaswa haswa kama kwenye misiba mingine. Hivyo ndivyo vijana walivyosahaulika pale kijijini.
Msimu wa kilimo uliofuatia ulianza na watu walianza kazi zao za mashambani kama ilivyokuwa kawaida yao. Ajuza akaongeza kukodi mashamba mara dufu. Wanakijiji walijishangaa kila wakiamka asubuhi walikuwa wachovu mno na hata wakati mwingine kuahirisha shughuli za shamba kwa siku husika. Lakini hata wangeamka kesho yake walijikuta wachovu zaidi ya ilivyokuwa jana.
Baadhi ya wanakijiji walijua labda uzee ulikuwa ukiwanyemelea. Lakini cha ajabu hata vijana walikuwa wakilalamika kuchoka sana tena isivyokawaida. Wanakijiji wakaanza kufa mmoja baada ya mwingine. Wakawa wakishauriana kupunguza ukubwa wa mashamba maana afya zao zilikuwa za muhimu kwa maendeleo ya kijiji. Lakini wapi bwana, uchovu ukawa kama sehemu yao ya maisha.
Ntemi alipata malalamiko na kuitisha mkutano wa kijiji na kuwaomba wanakijiji wake wapumzike kufanya kazi kwa wiki nzima labda mambo yangetulia. Wiki iliisha na watu walikuwa wachovu kila uchwao. Usiku mmoja Ntemi aliamka usiku wa manene na kutoka nje ya Ikulu, maana alisikia sauti ya mtu akitwanga kwa kutumia kinu. Alipotoka nje hakuona mtu anayetwanga bali alisikia sauti za vinu zaidi ya kimoja vikitwanga tena bila kupumzika.
Ntemi aliogopa kwenda kuchunguza na kupanga kwenda kumtafuta mganga kijiji cha pili maana aliona kama mauza uza na hakujua haswa ni nani aliyehusika na tukio hilo. Ntemi usingizi ulimpaa maana hata hao sungusungu wake anaowategemea hakuwaona kwenye doria ya usiku. Mawazo mengi sana yalimjia kichwani ikiwa ni pamoja na kumshuku mganga wa kijiji maana alikuwa amemkatalia ombi lake la kuutumia msitu wa tambiko kwa tambiko lake binafsi.
Asubuhi iliyofuata ilikuwa ya vituko zaidi maana wanakijiji wanne ambao hawakwenda shamba siku iliyopita walijikuta wanaamka na tope jeusi la majarubani. Wanakijiji wakaanza kulalamika kuchezewa. Kiongozi wa sungusungu pia akatoboa siri kuwa jeshi lake lilikuwa halifanyi doria za usiku kwa sababu wanakuwa wamechoka na wakisema wajipumzishe tu, huwa wanaamka kumekucha.
Ntemi aliamuru baragumu lipulizwe na watu wasogee eneo la mikutano ya kijiji. Ntemi alikuwa amefura sana hata kuongea kwake ni kama alijilazimisha tu. Aliwasimulia kuhusia na vinu vilivyokuwa vinatwanga usiku kucha. Hakuna aliyekuwa na taarifa au kukiri kuwa alikuwa akitwanga usiku. Aliamua kukitambulisha kikundi cha waganga maarufu kwa kuwakamata wachawi toka kijiji jirani.
Wanakijiji wa Kanyaga wakawa wanashangaa tu maana wamechoka na hawajui sababu za kuchoka kwao. Ngoma za kumsaka mchawi zikaanza kulia. Waganga wakacheza haswa mpaka nyasi walizokuwa wakizikanyaga zikakauka. Baada ya muda kiongozi wa ngoma akanyoosha mkono na ngoma pamoja na wachezaji vikasimama. Mganga akasema mizimu yake imemwambia kuna mtu anawachezea raia wa Kanyaga.
Kuna mtu mmoja anawalimisha raia wote kwenye mashamba yake ya mahindi na mpunga. Na pia huwa anawatwangisha na kuwasagisha watu usiku kucha ili awalishe misukule wake. Kwamba siku za mtu huyo zilikuwa zimefika kikomo. Akawaambia wakati ngoma zinapigwa kwa mara ya mwisho ajitokeze mara moja ili wawe na mazungumzo nae huenda wangemsamehe.
Ngoma zililia, waganga wakacheza mpaka jasho lakini hakuna aliyesimama kujisema kuwa ndiye mchawi. Mganga akavaa kofia yake yenye manyoya ya bundi na miiba ya nungunungu. Akaanza kuongea kuwa yeye alikuwa hamfahamu raia hata mmoja isipokuwa Ntemi tu lakini mizimu yake ilikuwa ikimfahamu kila mtu pale. Akjiwekea ugoro puani na kupiga mfululilizo wa chafya akaanza kukimbia kama mbwa mwenyekichaa kumtafuta mchawi.
Baada ya kuzunguka wanakijiji wote alijirusha kati kati ya wanakijiji na kumkamata ajuza. Ajuza hata hakuonesha dalili za kuogopa mwanzoni. Akampeleka mbele ya wanakijiji wote. Ajuza alikuwa amevaa kaniki yake, mganga akaivua na kupandisha blauzi yake juu. Looh! Ajuza alikuwa na rundo la hirizi na shanga kuzunguka kiuno chake. Mganga alizivuta shanga na hirizi kwa mkono wake wa kushoto na kuzikata. Kasha akaamuru wasaidizi wake wazichome moto pale pale.
Baada ya hapo wakati watu wanazidi kushangaa, mganga alimwamuru ajuza kuachama. Mganga aliongea maneno yasiyoeleweka halafu akaingiza vidole vyake chini ya ulimi wa ajuza. Mganga akaonekana kama akihangaika kushika kitu kilichokuwa kikitereza toka ulimini mwa ajuza. Mara akavuta kwa nguvu, watu wakaruka na kupiga mayowe. Maana alitokea koboko mmoja mrefu kimo cha mgaga ila mganga alikuwa amemshika kichwa chake kwa nguvu na kumuua.
Mganga aliomba kipande cha chupa na kukitumia kumnyoa ajuza nywele zake. Alipomaliza kumyoa akaomba dawa ya unga iliyokuwa kwenye kikopo kidogo na kuupaka upaa wa ajuza. Akatangaza kuwa ajuza yule endapo angeurudia uchawi au kuficha kitu cha uchawi angekufa palepale mkutanoni. Akamwamuru ajuza aseme mbele za wanakijiji ni wapi alikuwa ameficha uchawi wake mwingine.
Ajuza hakuwa mbishi akasema upo nyumbani kwake. Mganga akasema ajuza yuko sahihi twendeni mkaone mambo ya ajuza. Watu walishikwa na butwaa kuona ajuza waliyemwamini na kumuona kimbilio wakati wa shida zao kumbe alikuwa mchawi wa kupindukia. Waliowahi kula chakula kwa ajuza walikuwa wakijaribu kujitapisha bila mafanikio.
Walipofika nyumbani kwa ajuza watu wengi walijaa mlangoni pa nyumba ya ajuza wakisubiri kuingia kujionea uchawi wa ajuza. Lakini mganga alipokuja aliwaomba wakae mbali ka mita mia maana kulikuwa na hatari mule ndani. Wanakijiji kusikia hatari walikaa umbali wa mita mia tatu hivi. Ajiza akafungwa kamba kwenye mzambarau wake hata hakuweza kujitikisa. Mganga alivaa kofia yake na kuanza kuizunguka nyumba huku akiinyunyizia dawa.
Baada ya zoezi la kuizunguka nyumba mganga alienda mlangoni na kumwaga dawa nyingi pale mlangoni. Mganga aliupiga teke mlango na kusema ‘‘Fumagako.’’  Walianza kutoka fisi waliokuwa wanakimbia kawa wamewashwa moto mgongoni. Wanakijiji walikuwa wakihesababu tu mpaka wakafika fisi mia tano na themanini. Mara ghafla bundi nao wakaanza kutoka kwa vurugu zote. Wanakijiji walishindwa kuwahesabu bundi kwa sababu walikuwa wanaruka bila mpangilio.
Mara chatu akaonekana akijisukuma kutoka nje, watu wakataka kumenya mbio lakini alipofika jirani na mlango na kuigusa ile dawa ya mganga aliyeyuka. Palipokuwa kimya mganga akamuita Ntemi wakaingia nae ndani na mganga akamuonesha kitu Ntemi lakini Ntemi hakuwa anaona kitu. Mganga akachukua dawa akampaka machoni, mara Ntemi akaduwaa.
Walipotoka nje tu, watu walikuwa wamejaa mlangoni. Ntemi uzalendo ukamshinda akasema jamani wale watu waliopotea na waliokufa tukawazika wamo humu ndani. Watu wakajawa na shauku ya kuwaona. Mganga alikuwa mstaarabu akawaambia kwa sasa sio watu tena bali ni misukule. Hawawezi kuishi kama binadamu tena kwa sababu wamekatwa ndimi na wanatisha sana. Nitafanya dawa ili waende kwenye makaburi yao. Wananchi wa Kanyaga hawakuwa wakatiri ila ajuza huyu aliwaamshia hasira kali sana. Mganga alikuwa mtu mstaarabu sana akawaambia kwa sababu wamesha muadhibu ajuza yule ilikuwa haina haja ya kumdhuru. Wanakijij walimbeba ajuza mzega mzega na kwenda kumtupa nje ya mipaka ya kijiji cha Kanyaga. Wakampa onyo kuwa sasa hivi wamemuacha hai ila akirudi tena kijijini watakuja kuitupa mifupa yake pale mpakani ili iwe fudisho kwa wachawi wengine.

HADITHI YA 7: NJAA KALI YAIKUMBA KANYAGA
Baada ya kumfukuza ajuza mchawi toka kwenye mipaka ya kijiji cha Kanyaga, wanakijiji walianza kulala kwa raha mustarehe. Baadhi ya wanakijiji waliamua wafidie usingizi kwa siku ambazo walikuwa wakitumikishwa kwenye mashamba ya ajuza mchawi. Akili ya mwanadamu imeumbiwa kusahau, ajuza akasahulika kabisa pale Kanyaga. Maisha yakarudi kama ilivyokuwa awali, watu wakawa wakiamka alfajiri kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli za mashamba yao.
Lakini kwa bahati mbaya sana msimu huu haukuwa na mvua za kutosha. Mwanzoni mwa msimu mvua zilianza kunyesha vizuri na wakulima wa Kanyaga wakalima na kupanda mazao yao. Wakawa wakiyapalilia ili kuondoa magugu yaliyokuwa yakiisumbua mimea isikue kwa usahihi. Kila mkulima alikuwa amemaliza palizi ya kwanza na wakawa wanasubiri palizi ya pili ambayo ndio ilikuwa palizi ya mwisho na ya muhimu sana.
Palizi ya pili ilikuwa ni ya muhimu kwa sababu ilisaidia mimea kubeba watoto wenye afya zaidi. Wakulima walikuwa wakiisubiria palizi ile ije bila mafanikio. Maana jua lilikuwa kali kiasi cha kuanza kukausha mazao na magugu madogo madogo yaliyokuwa yameanza kuota. Wakulima wa Kanyaga wakaanza kutia hofu kama msimu ule ungeleta mazao ya kutosha maghalani mwao.
Mara moto wa ajabu ukavamia mashamba yao. Ukaunguza kweli mahindi na karanga zilizokuwa mashambani. Moto ukaingia msitu wa jirani na kijiji na ukawa ukiimba usiku na mchana na miti ya mwituni. Siku ya tatu moto ukavuka msitu na kufika sehemu kulipokuwa na majaruba ya mpunga. Huko nako kukawa na kilio kwa wakulima wa Kanyaga. Moto ulipo kula sehemu kubwa ya mpunga ndipo uliamua kuzimika wenyewe.
Ntemi Nchemu akaamua kuitisha bunge la wazee na kujadili muongozo wa kusaidia jamii nzima ya Kanyaga. Wazee wenye mvi zao wakamshauri Ntemi, kuwambia wakulima watafute mbegu za mihogo na marando ya kutosha ili waweze kupata japo chakula cha kuwafikisha msimu ujao wa kilimo.
Ntemi aliwakusanya wanakijiji wake kwa baragumu na kuwaasa watafute mbegu za mihogo na marando na wazipande. Halafu Ntemi na viongozi wake wangeenda kutambika kwa ajili ya kupata mvua. Wanakijiji wakaanza msako wa mbegu za mihogo kuanzia ile michungu hata ile iliyo mitamu kwa hofu ya njaa. Hakuna mwanakijiji aliyekuwa na ujasiri wa kutaka kuishuhudia njaa. Marando yalileta ugumu kupatikana pale kijijini kwa sababu wengi walikuwa hawapendelei kula viazi vitamu. Hivyo basi kila mtu kwa wakati wake alikuwa akitembelea kijiji cha jirani na tela lake kwa ajili ya kuomba marando ya viazi.
Wakalima matuta kama walivyoelekezwa na kupanda mbegu za mihogo na marando ya viazi. Kila mkulima alipomaliza kulima na kupanda kwa kadiri alivyoweza basi Ntemi akaongoza wazee kwa ajili ya tambiko la mvua. Mvua kubwa ilinyesha siku ile na watu wakafurahi kujua kuwa angalau wangeambulia mihogo na viazi. Mvua ziliendelea kuwa za mfululizo na kusaidia mazao kwenda vizuri bila ya bugdha.

Mpunga pia ambao haukuungua ulirudi katika hali yake na ukabeba masuke yake. Lakini mpunga haukuwa mwingi sana wa kukidhi mahitaji ya kijiji kizima. Watu wengi walipungukiwa chakula cha akiba kwa kasi na wakawa wakiombea viazi vikomae waanze kuvila. Viazi huwa havichelewi baada ya majuma kumi na sita tu kila mwana Kanyaga akawa akishikilia kiazi cha kuchoma, cha kubanika au cha kuchemsha.
Wana Kanyaga walikula viazi haswa mpaka vikaanza kuwakinai. Na ubaya wa viazi vitamu bwana huwa havitunziki shambani. Baada ya miezi miwili toka vikomae vikaanza kushambuliwa na wadudu waliokuwa wakivibugua. Panya bubu nao hawakuwa nyuma wakaanza kupita chini kwa chini, tuta hadi tuta wakibuguna viazi vitamu. Ishara ya panya buku ni rahisi tu ukikuta udongo tifutifu shambani kwako matuta matuta ujue yuko kazini.
Walinyeshewa na mvua nyingi ikabidi kutoa elimu. Wazee hao walidai njaa kama hiyo iliwahi tokea kijiji cha mbali cha Ntemi Mahinyila. Wanakijiji wa ntemi Mahinyila walilima viazi na vikaanza kuharibiwa na wadudu waharibifu. Mizimu ikamfundisha namna ya kutunza chakula kwa njia salama. Aliwaamuru wanakijij wake wavune viazi vyote na wakavimenya. Akawaamuru wachukue mapipa na kuvichemsha. Kisha wakavianika juani. Jina lililopendezwa na mizimu ni Matobolwa, mpaka leo hii wanakijiji wale wanatengeneza matobolwa kama kumbukumbu yao.
Hiyo ilikuwa kijiji cha Mahinyila, na hapa tuko Kanyaga. Wazee walishauri viazi vyote vimenywe na kukatwakatwa vipande vidogo vidogo. Kwa sababu viazi vingetenezwa kwa aina moja vingewakinai watumiaji, mizimu ilipendekezwa vingine vianikwe kwenye mawe mpaka vitakapo kauka na vitaitwa Michembe.
Wana Kanyaga walitengeneza Michembe na Matobolwa kwa kadiri walivyoweza. Na kila mtu alitunza katika ghala yake. Wanakijiji walikuwa wakinywa uji au ugali wa Michembe kwa maziwa mgando kila uchwao. Wengi walikikinai kile chakula lakini walikuwa hawana chaguo linguine. Hivyo wengi waliamua kunywa mtindi tupu au hata kushinda njaa ili wapate hamu ya kula michembe au Matobolwa usiku.
Njaa ilizidi kuwa kali, wanakijiji wakajikuta wakiachana na desturi ya ukarimu kwa sababu maghala yalikuwa hayana vyakula. Ulikuwa ukimtembelea rafiki yako au ndugu yako hata kama alikuwa na ratiba ya kupika na kula alikuwa akikusubiria uondoke ndipo apike na kula na ndugu wa nyumbani kwake tu. Njaa ikaleta utamaduni mwingine na watu wakaupokea. Hakuna aliyediriki hata kubeba ujauzito kwa sababu ya njaa.
Njaa inaweza kuugeuza mzimu mwema kuwa shetani, wanaume waliambizana walipokuwa wakicheza bao. Kuna mwanaume alienda kumtembelea rafiki yake na akakuta chungu kipo kwenye mafiga na kwa makadirio usingepita muda mrefu bila ya chakula kupakuliwa. Lakini cha ajabu, mama wa familia akakaa mbali akisubiri mgeni aondoke. Alipoona mgeni haondoki akachuku maji akaweka kwenye kalai, akayapooza na kuanza kwaogesha watoto mchana wa jua kali.
Njaa uwe unaisikia tu kwenye hadithi. Njaa ni mwanaharamu anayekera na hauwezi kumuondoa akikuvamia. Hata watoto waliokuwa wakijifunza kutembea walijua kuwa njaa ilikuwa imewatembelea. Maana hakuna mtoto aliyekuwa akibembelezwa kula. Sufuria la uji wa Miichembe lilikuwa likigombaniwa na wakubwa kwa watoto.
Maghala mengi yakaishiwa chakula. Watu wakaanza kuwa wehu wakijiongelea tu wenyewe njiani. Ngombe na watu walikonda mpaka mbavu zikafanan na nyuzi za zeze. Familia zenye mifugo wakaanza kuchinja ng’ombe na kumkausha ili awe anawasukuma kwa muda mrefu. Wasio na mifugo wakawa wakikopa mbuzi kwa wenye mifugo kwa ahadi ya kurudisha magunia matano ya mahindi baadae.
Njaa rafiki yake mkubwa ukame. Basi ukame akaja kumsaidia rafiki yake kazi ya kuwanyoosha wana Kanyaga. Wanakanyaga walinyooshwa na wakanyosheka haswa. Wazazi wakaanza kuchukia salamu za asubuhi kwa kuona ni kelele tu masikioni mwao. Mabwawa ya maji ya kijiji yalikauka yote. Wanawake wakawa wakifuata maji maili nyingi na kurudi kwa kuchelewa.
Maji yaliadimika hata vijiji vya jirani kwa hivyo yakaanza kufuatwa mbali tena kwa matela ya ng’ombe. Mabinti wengi waliolewa kwa ajili ya umbali wa kufuata maji. Wengine sahani ya ugali kwa uadimu wake iliwafanya wahamie kwa wavulana wa kijij kile. Miwa pia iliwasababisha mabinti wengi waolewe kwa muda au jumla.
Hakuna mtu aliyeheshimika kama mwanamke wa Kanyaga. Licha ya shida zote hizo lakini hakuwepo hata mmoja aliyediriki kusaliti ndoa yake kwa sababu iwayo yoyote ile. Walikubali kurudi hata usiku wa manane ilimradi waje waihudumie familia yao hata kama ni kwa kuchelewa. Wanaume wa Kanyaga walikuwa wakicheza bao, kupiga soga na kunywa pombe ya mkopo tu.
Ntemi aliita wazee wa bunge lake na kwenda nao kwa ajili ya tambiko la mvua ili watu angalau wapate maji. Tambiko lilikuwa la mafanikio lakini maji bila chakula maisha bado yalikuwa magumu. Kwa bahati nzuri wachungaji walirudi na uyoga uliokuwa umeota katika pori la kijiji. Basi kila mtu akakimbilia kutafuta uyoga porini. Wana Kanyaga wakarudi na mafurushi ya uyoga na kuuchemsha ili uwe kitoweo cha siku ile. Uliobaki ukaanikwa juani ili usioze.
Mabalaa huwa hayabishi hodi baadhi ya wana Kanyaga walichuma hadi bhobha, ule uyoga wa njano. Uyoga huu huwa na vituko sana, maana kuna wakati watu hula lakini hauwaletei shida yoyote. Lakini kunawakati huwaendesha watu, kuleta kizunguzungu na kutapika pia. Wengi wa wataalamu wa uyoga waliuepuka hata kwa matumizi. Lakini sasa ilikuwa njaa na hauna uchaguzi mwingine. Ni kula bhobha au kushinda na njaa. Wengi waliona ni bora kula na kujisikia kizunguzungu kuliko kushinda na njaa.
Kila mwanafamilia jioni ile alikuwa ameshikilia bakuli la uyoga akila la kufurahia radha tofauti ya chakula. Mara baada ya dakika kadhaa hivi wale waliokula bhobha wakaanza kujisikia kizunguzungu. Wengine wakawa wakitapika tu. Baada ya muda povu jeupe likaanza kuwatoka mdomoni na puani. Kesho yake asubuhi waliokula ule uyoga wengi walikufa isipokuwa mtoto mdogo wa Ntemi Dongwe tu. Yeye hata hakulalamika maumivu ya tumbo.
Kulikuwa na msiba mkubwa sana pale Kanyaga. Wanasema msiba wa wengi ni sherehe lakini hapa Kanyaga watu walikuwa wakilia sana kwa sababu hata chakula cha kupika msibani hakikuwepo. Hata baada ya msiba walikuwa hawajui wangekula nini. Watu waliwaombolezea ndugu jamaa na marafiki zao huku wakikosa hata nguvu ya kuendelea kulia kwa sababu ya njaa. Walizika kwenye makaburi yaliyokuwa karibu karibu ili kuepuka kuwachosha watu.
Msiba haukuombolezwa siku nyingi maana watu walikuwa wakichakalika kutafuta chakula kwa ajili walio hai. Wakagundua kuwa mihogo ya kisamvu licha ya sumu yake lakini inaweza lika kama ingelowekwa kwenye maji kwa siku kadhaa. Maana mihogo inayoliwa ilikuwa hata haina dalili ya kukomaa. Basi watu wakahamia kwenye mihogo ya kisavu mpaka visamvu vyote vika kauka. Njaa ilizidisha mara dufu makali yake.
Watu walibadilika sura kwa kukonda wakaanza kufanana na vikaragosi. Wanaume wengi walizitoroka familia zao na kukimbilia kusikojulikana maana waliona ni bora wasikie familia zao zimekufa kuliko kushuhudia wakimpoteza mwana familia mmoja baada ya mwingine. Wakina mama walisima imara kuzitetea roho za watoto wao zivuke salama msimu ule wa njaa kali.
Ntemi alikuwa hajawahi kusikia kuwa mizimu ingeweza kuleta chakula na watu wakala, hivyo hata alipoombwa kwenda kuiomba mizimu hakujua akaombe nini. Alitulia ikulu kwake akiwa na huzuni na machungu makubwa mno maana hata baadhi ya wazee wake wa baraza walikuwa wamezitoroka familia zao. Ntemi kwa moyo wa unyonge alimuomba kijana wake Dongwe aongozane nae ili wakatoe tambiko. Dongwe kijana mdadisi alifurahi kwenda kudadisi msitu wa matambiko.
Dongwe alikuwa ameshika kamba ya mbuzi alikuwa amekonda lakini akifananishwa na mbuzi wenzake ndiye aliyekuwa mbuzi mnene kuliko wote. Dongwe na baba yake wakaelekea msitu wa tambiko, haukuwa unatisha kwa sababu ya ukame uliopukutisha majani yote. Hivyo Dongwe akakaa mbali akimuangalia baba yake akifanya tambiko. Alipomaliza tu kufanya tambiko akaangalia juu na kuiamuru mvua ya Amani inyeshe kama tambiko limekubaliwa.
Mvua kubwa ilishuka, Dongwe na baba yake wakashika njia kuelekea nyumbani. Walipofika nyumbani tu. Makundi ya senene na kumbikumbi yalitua katika mipaka yote ya Kanyaga. Wana Kanyaga hawakujali mvua tena wakatoka na makapu, ndoo, magunia na chochote ambacho kingeweza kutunza kumbikumbi na senene wale. Watu walikuwa wanazoa na kwenda kumwaga ndani shehena na kumbikumbi na senene. Wanakijiji walibeba senene mpaka wakachoka lakini kumbikumbi na senene walikuwa hawapungui. Na hivi ndivyo kanyaga ilivyopona toka kwenye baa la njaa.

HADITHI YA 8: BODO NA LAANA YA MIZIMU
Mila na desturi za Kanyaga ni kitu pekee ambacho wanakijiji wote waliviheshimu na kuvifuata bila ya kuhoji wala kutilia shaka. Wanakijiji wote wadogo kwa wakubwa walikuwa wakifuata mila na desturi kwa unyenyekevu wa hali ya juu. Unyenyekevu huu ulikuwa ukirithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine. Wana Kanyaga walikuwa wakiamini kuwa hata mafanikio waliyo nayo ni kwa sababu ya kufuata mila na desturi zao kwa ufasaha.
Mila na desturi hizi zilikuwa zikifundishwa katika kila kaya wakati wa kuota moto wa jioni. Kwa sababu vijana wa kiume walikuwa wakilala nje kwa ajili ya kulinda mifugo basi wao walipata mafunzo Zaidi kuliko wasichana. Mvulana alikuwa akizaliwa baba wa familia. Ilikuwa mwiko kwa mwanamke kumwita kijana wa kiume mtoto hata kama ni wakumzaa. Kama umekosa jina zuri basi ita Ngosha, hata kama anajifunza kutembea. Hata hivyo kanyaga walikuwa na mfumo dume ambao ulikuwa ukilenga kumuelimisha Zaidi mtoto wa kiume ili awe kichwa cha familia bora baadae.
Waliokuwa wanastahili kuitwa watoto ni wasichana tu. Watoto wa kike elimu yao ilikuwa rahisi naya kuchosha. Maana walikuwa wakifundishwa kuandaa na kutenga chakula, kupiga magoti wakati wa kukabithi maji ya kunywa na kusalimu. Mgeni alikuwa akifika msichana wa familia anakimbilia jikoni kupika bila kumuuliza mgeni kama ameshiba au amekula alikotoka.
Mila na desturi ziliwajenga vijana wa kike na Mangosha wakawa watu bora wa jamii ya Kanyaga. Kila mmoja wao alipenda kufanya vile alivyofundisha mbele ya wazazi ili asifiwe na kuonekana hodari wa kuzingatia mila na desturi za Kanyaga. Wazazi wa Kanyaga walikuwa wazazi wa kila kijana na Ngosha. Walikuwa hawawezi kuvumila kuona ati mtoto akienda kinyume na mila na desturi. Ulikuwa ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha kila kijana na Ngosha anaenenda sawa sawa na mila na desturi za Kanyaga.
Lakini kila jamii licha ya ubora na muelekeo mzuri wa mila na desturi huwa wanajitokeza vichwa ngumu. Wale wanaojifanya wana masikio ya kufa. Wazazi wakizungumza jambo linaingilia sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto. Hata uwatendee wema kiasi gani wao ukengeufu ndio uchaangamfu wao. Kila jamii lazima awepo lau mmoja au kikundi. Na kama katika jamii yako hayupo mkengeufu, hebu jichunguze wewe mwenyewe uone.
Katika kijiji cha Kanyaga alikuwepo kijana aliyeitwa Bodo. Huyu aliamua kuwa mkengeufu na asiyeelewa somo wala fundisho toka kwa mtu mzima. Alikuwa akipenda kutumia lugha ya matusi tu muda wote. Ijapokuwa alikuwa akichunga mbuzi, na usumbufu wa mbuzi unafahamika lakini yeye alitia fora.
Bodo alianza kama utani hivi. Siku moja aliligundua jina la utotoni la mama yake kuwa alikuwa akiitwa Ngolo. Basi Bodo akawa akimvizia baba yake akitoka tu kwenda kucheza bao au kunywa pombe basi alikuwa akimuita mama yake kama mdogo wake. Maskini mama Bodo alikuwa mama mpole kweli, alikuwa akiishia tu kusema ‘’sipendi uniiite hilo jina nitakuchapa.’’ Kwa sauti ya upole kama alikuwa akimbembeleza kulala.
Utukutu wa Bodo ukaanza kuota mizizi, akawa akiwavizia mabinti wadodo wadogo waliokuwa wakienda kuteka maji wakati wa jioni na kuwatishia kwa kulia kama fisi kwenye vichaka vya karibu. Basi mabinti walikuwa wakikimbia na kuvunja mitungi ya maji. Halafu Bodo hujitokeza toka kichaka cha jirani na kuwacheka mpaka akawa akigala gala chini.
Bodo akaendelea kupamba moto, akawa akivizia wasichana waliokuwa wakichunga ndama porini na kuwalazimisha kufanya kile alichokitaka huku akiwapiga pale walipokuwa wakimkatalia. Mabinti wengi walikuwa wakirudi kabla ya wakati nyumbani wakilia na kumlaumu Bodo kwa ukatili wake. Bodo akawa akijificha porini na kurudi nyumbani giza likiingia. Wazazi wake walipomuuliza kuhusiana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili, Bodo aliruka maili mia mbili.
Bodo akaanza ujanja mwingine. Alipokuwa akienda kuchunga ng’ombe na njaa ikamlemea basi alianza kuiba mahindi, viazi vitamu, mihogo, na karanga toka kwenye mashamba ya watu. Alikuwa akirudi toka machungani, alikuwa hali chakula alichobakiziwa na kudai kuwa rafiki zake walikuja na gudulia ya maziwa ya mgando hivyo alikuwa bado ameshiba. Mashitaka yalipoletwa, Bodo kama kawaida yake akakana.
Siku moja wakati wa kiangazi alibeba kijinga cha moto kwa uficho wakati akienda machungani. Alipofika machungani akaiba viazi vya watu akavila na kuanza kuchezea moto. Alikuwa akiwasha moto kwenye majani makavu na kuuzima kwa miguu yake kwani alikuwa amevaa makatambuga. Aliwasha mara ya mwisho ili aende kuwarudisha mifugo aliokuwa anachunga maana walikuwa wameingia kwenye shaba la mahindi la jirani. Alipouwasha moto na kujiziuka kuangalia ng’ombe upepo ukavuma ukaukoleza moto. Alidua mara kadhaa na makata mbuga yake moto ukamzidi uwezo.
Kwa sababu alikuwa na akili nyingi akawaswaga ng’ombe kuelekea nyumbani kwa mwendo wa mchakamchaka. Watu walimuuliza leo kulikoni alidai alikuwa akisumbuliwa na jino hivyo alikuwa akiwahi kuchimba mzizi wa mpapai. Alifika nyumbani na kuwafungia mifugo zizini na kujitupa kwenye ngozi ya ng’ombe na kujifanya mgonjwa mahututi. Baada ya muda wana Kanyaga wakaona moshi mzito ukitokea katika msitu wa kijiji.
Walifanya maalifa ya kuuzima lakini hawakuweza. Hivyo waliamua waende kukata miti ya mbele iliyokaribiana na msitu wa tambiko ili kuuzuia moto usijedhuru msitu wa tambiko. Walifanikiwa kuuzuia moto kwa namna ile. Msako wa kumtamfuta baradhuri aliyefanya ule uhalibifu ulifanywa lakini bila mafanikio. Kila waliyemuuliza alisema hajui, hata Bodo mwenyewe alisema hajui maana jino lilikuwa likimsumbua sana. Wazee wengi walilaani kitendo kile maana mizinga yao ya nyuki iliungua na kuwasabababishia hasara kubwa.
Yeye Bodo akawa akiboresha tabia mbaya kila uchwao. Safari hii alikuwa akipita karibu na bwawa la maji mida ya kupunga kwa kua, akakutana na mabinti wakioga. Basi akatafuata kichaka na kuanza kuwachungulia. Kila ikifika jioni basi huenda kujibanza kwenye kichaka na kuwachungulia wasichana waliokuwa wakioga. Na mbaya Zaidi alikuwa akikutana nao mmoja mmoja alikuwa akiwaambia hadi nguo za ndani walizokuwa wamezivaa. Wasichana wengi walimkasirikia Bodo na hata kumripoti kwa mama yake. Lakini mama yake Bodo alikuwa akimtishia tu kumchapa.
Kuna siku moja mzazi mmoja alimkuta Bodo akimtukana binti ambaye alikuwa ametoka kuchota maji. Mzazi alipouliza kulikuwa na nini mpaka malumbano yao yakageuka kuwa matusi. Kumbe Bodo alimchungulia binti yule wakati akioga na akamwambia nguo zake za ndani binti alipojaribu kukoroma Bodo akaanza kuporomosha matusi. Basi yule mzazi akachukua jukumu la kumuadhibu Bodo.
Bodo baada ya bakora mbili za makalioni kumuingia kisawa sawa, akageuka kuwa mbogo. Akaamka akaidaka fimbo na kuivunja vunja. Mzazi akaamua aanze kumzaba vibao, Bodo akampiga mweleka mmoja mzazi puuuu chini. Bodo akamkalia kifuani akampiga ngumi na kumwagia mchanga machoni kisha akamenya mbio msituni. Alikaa msituni kama siku tatu, wazazi wake wakabidi wamfuate na kumuahidi kuto muadhibu endapo angerudi nyumbani.
Wazazi wengi walilaani kile kitendo kwani kilivunja heshima ya wazazi kwa watoto pale kijijini. Wazazi wa Bodo wakaomba msamaha ikiwa ni pamoja na kulipa mbuzi wawili kama masumule, fidia ya adhabu. Bodo hakupunguza mapepe yake bali alizidi na kuwa mbishi Zaidi kwa watu wazima. Siku moja baada ya kikao cha Ntemi na wanakijiji likapangwa tambiko la Amani ya kijiji. Bodo akawanong’oneza vijana wenzake kuwa angeenda wachungulia wazee pale walipokuwa wakifanya tambiko ili nayeye awe anajifanyia matambiko yake.
Vijana walijaribu kuwapasha habari wazazi kutokana na mpango wa Bodo, kwa sababu mila na desturi zilikuwa wazi hakuna aliyetilia maanani kuwa Bodo angeenda. Mila na desturi zilikuwa zikikataza mtu asiyehusika na tambiko kuhudhuria au hata kuchungulia tambiko. Kimsingi hakuna aliyekuwa akiruhusiwa kuingia katika msitu wa tambiko hata kama ni muhusika siku tofauti na siku ya tambiko. Kwa sababu kukiuka hivyo ni kujitafutia laana ya mizimu.
Siku ya tambiko ilifika, wahusika wakaongoza njia kuelekea msitu wa tambiko wakiwa na mahitaji yote ya tambiko. Bodo nae akafungulia mifugo kama anaenda kuichunga vile, kumbe moyoni mwake alikuwa akipanga mipango yake. Moyo wa mtu ni msitu mnene. Wazazi wa Bodo hawakugundua mpango wa mtoto wao. Bodo akafika machungani, safari hii alienda karibu na msitu wa tambiko ili kutimiza azima yake. Akawaacha mifugo wake na kuanza kunyata kwa hatua ndogo ndogo.
Aliwaona wazee na Ntemi wakiwa na maandalizi ya tambiko, kwa sababu msitu ulikuwa ni mnene basi Bodo akajibanza kwenye kichaka cha karibu ili ashuhudie vizuri. Wazee wakaanza kuvua nguo huku ngoma zikipigwa kwa kasi sana. Mara ya kwanza Bodo alidhani wanavua mashati tu. Akatahamaki kuona walianza kuvua na suruari zao. Bodo akatulia kwenye kichaka chake ili ashuhudie vyema. Mara wazee wakavua nguo zote wakawa wakicheza kuzunguka mti wa tambiko. Bodo baada ya kuona hakuna hatari yoyote na wazee walikuwa wakizunguka tu mti wa tambiko, ujinga wake ukamjia. Akasema aondoke aende kuchekea mbali kwani ameshashuhudia kila kitu.
Bodo akainuka akaanza kunyata ili aondoke mazingira yale na kwenda kuangua kicheko chake mbele ya safari. Alipiga hatua ya kwanza tu, radi ilisikika kwa kishindo kikubwa katika kichaka alichokuwa amejificha. Ntemi aligeuka kuona kuna nini akaona vipande vya nguo vikiruka kila kimoja upande wake. Na wakati ule ule radi pia ilipiga nyumbani kwa kina Bodo na kuwauwa baba yake na mama yake pale pale. Tabia mbaya ya Bodo ikagharimu maisha ya wazazi wake.

HADITHI YA 9: MKUTANO WA AKINA MAMA.
Mwanamke ni nguzo ya familia yoyote ile, iwe familia ya wastaarabu au hata familia ya mabaradhuri. Mwanamke ndiye kiumbe pekee mwenye uwezo wa kuitengeneza au hata kuibomoa familia na jamii yake. Mvuto wa mwanamke haupingiki kwa hoja iwayo yote ile kwa sababu akiamua kuiangamiza familia yake ni muda mfupi tu wanafamilia wataacha majina yao na kuitwa malehemu. Ratiba ya mwanamke ndiyo ratiba ya familia nzima. Maana kila apangapo ratiba hufikilia hisia na matakwa ya kila mwanafamilia.
Wanaume wengi wa Kanyaga walikuwa hawajui watakula mlo gani kila kukipambazuka. Lakini kwa wanawake ilikuwa jambo dogo na hata walikuwa hawaliwazii kabisa. Walipokuwa wakitenga chakula kila mtu alijikuta akipata mboga ya mahitaji yake. Kuna ambao hawakupenda kula mrenda walikuwa wakitengewa maziwa ya mgando kila mrenda ulipokuwa ukipikwa. Kuna wengine walikuwa hawapendelei maziwa hivyo mboga zikikosekana basi kulikuwa na nyama ya kukaushwa iliyohifadhiwa kwa muda mrefu darini, maarufu kwa jina la Ng’omele. Kila mwanafamilia alikuwa akiridhika kila chakula kilipotengwa.
Ratiba za kuanza msimu wa kilimo pia zilikuwa zikipangwa na wanawake wa familia. Haijawahi kujulikana walipata wapi utashi huo lakini kila walipofanya maaamuzi ya zao la kulimwa kwa wingi walikuwa sahihi. Wanaume wengi walikuwa wakijivunia tu magunia yaliyorundikwa gharani bila hata kuwapongeza wake zao kwa juhudi waliyokuwa wakionesha.
Baadhi ya wanaume walevi walikuwa wakipanga masharti magumu kwa wake zao. Kwa mfano walikuwa wakitaka kila waliporudi toka ulevini wawakute wake zao hawajalala hata kama ni usiku wa manane. Wengine walidai chakula cha moto na kuwalazimisha wake zao kuamka usiku na kuanza shuruba za kupika chakula kwa ajili yao. Wengine walienda mbali Zaidi kwa kuwageuza wake zao kuwa ngoma na kuhakikisha wakizipiga kila waliporudi toka ulevini.
Lugandya, mlevi maarufu pale Kanyaga alikuwa ni kinara wa kumyanyasa mke wake, Nkwaya kwa vipigo. Alikuwa akilewa hurudi na kumlaumu kwa nini hakumpatia mtoto. Walevi huwa hawana akili kabisa kwa sababu anaweza kukuuliza swali ukajitahidi kumjibu vizuri yeye akakwambia umemdharau. Basi mkewe Lugandya akawa ngoma ya kijiji haswa. Kila jioni ni vipigo na mayowe. Siku moja Lugandya akamwambia mke kuwa anataka kumuolea mke mwenza kwa sababu yeye tumbo lake lilikosa shukrani.
Nkwaya binti Machota alikuwa ni mke mnyenyekevu kwa mumewe, akapiga magoti na kumuomba wajitahidi kufuata masharti ya mganga kwa mwaka mmoja asipompatia mtoto basi aoe mke mwingine. Weee! Sijui maneno gani yaliingia masikioni kwa mlevi Lugandya. Alimuangushia kipigo cha kiutu uzima. Akachukua mwichi wa kutwangia akaanza kujpiga nao. Nkwaya ilibidi apige yowe za kuomba msaada. Majirani walifika kutoa msaada na kumkuta Nkwaya akiwa na hali mbaya.
Walimchukua Nkwaya na kwenda kumpeleka kwa mganga wa jadi usiku uleule. Mganga alipomchunguza mgonjwa wake akagundua alikuwa amevunjia mguu na mkono na alikuwa akitokwa na damu puani na mdomoni. Mganga alitumia miti shamba yake kwa usahihi na kuzuia damu iliendelee kutoka Zaidi. Asubuhi iliyofuata mke wa mganga, Mhoja akaanza shughuli ya kutibu mkono na mguu wa Nkwaya vilivyovunjika. Utaalamu wa kuunganisha mifupa iliyovunjika Mhoja alichanjiwa na baba yake Nyenye.
Hivyo mganga japokuwa alikuwa akijua miti shamba ya aina zote lakini alikuwa hajapata bahati ya kuchanjiwa dawa ya kuunga mifupa. Mganga alikuwa ni mtu mwenye jaziba sana hivyo alikataliwa kuchanjwa dawa ya kuunga mfupa iliyovunjika kwa sababu mtu aliyechanjiwa dawa ya kuunga mifupa alikuwa akimpiga mtu kibao au hata ngumi basi mtu yule aliyepigwa huanza kuoza sehemu aliyopigwa. Hivyo waliokuwa wakichanjwa dawa ile ni watu wapole na wasio na hasira za karibu.
Nkwaya alipofikisha siku saba akaanza kufanya mazoezi ya kutembea na kuuonyoosha mkono wake baada ya kupona tu, wazee waliitisha mkutano wa kijiji na kumuuliza Lugandya sababu ya kutaka kumuua mkewe. Lugandya alikuwa hana cha maana cha kueleza umma wa Kanyaga kwa hiyo alichapwa viboko arobaini mgongoni pamoa na kulipa masumule ya ng’ombe mzima ili watu wale kabla ya kumkabidhi tena mke wake. Lugandya alitii na kutekeleza aliyoambiwa.
Lakini wengi wa wanawake hawakuridhishwa na adhabu aliyopatiwa Lugandya kwa sababu alikuwa amekusudia kuua. Kwa maono yao waliona apokonywe mke ili watu wengine wajifunze kuheshimu wake zao. Lakini hakuwepo wa kuyaeleza mawazo hayo mbele ya umma wa wanaume wanyanyasaji. Moja kati ya wanawake ambao hawakuridhishwa na kitendo cha kinyama alichokifanya Lugandya alikuwa ni Malkia. Hivyo baada ya kuyatambua mawazo ya wanawake wenzake na hali kandamizi waliyokuwa nayo wanaume wengi pale Kanyaga, akatangaza mkutano wa wanawake ambao ungefanyika kesho yake Ikulu.
Wanawake wengi walipiga makofi na vigeregere kuona Malkia ameamua ambacho wengi wao walikuwa wakitamani kwa muda mrefu. Baadhi ya wanaume walihoji maada ya mkutano ila walijibiwa ni mambo ya wanawake na ndio maana ya mkutano wa wakina mama la sivyo wangeweza kuelezea palepale tu. Wanaume walifyata mikia yao na kujipa matumaini wake zao walikuwa watiifu na wasingeweza kuwaza kupindua familia zao.
Siku ya mkutano kwa Ntemi pakawa hapatoshi. Maana wanawake walikuja kwa idadi yao kamili. Hata ambao siku iliyopita walidamkia mashambani leo walikuwa wakwanza kufika na kukaa nafasi za mbele kabisa. Wanawake waliamua kubanana na kutosha sehemu ile ile iliyokuwa ndogo. Vicheko, nderemo na vifijo zilijaa pale kwenye mkutano. Kila mwanamke alikuwa anafuraha kuona hata wanawake waliokuwa wakisemwa ni wapole leo walikuwa wakiongea kwa furaha na vituko.
Malkia alisimama na kuowasalimia, ‘‘Wanawake wa Kanyaga hoyeee!’’ wanawake walijibu kwa bashasha na furaha kubwa, ‘hoyeee.!’’ Malkia aliwashukuru kwa mahudhurio ambayo hata hakuyategemea. Aliwaasa wanawake kuwa wito wake haukuwa jaribio la kupindua uongozi wa waume zao bali kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa wanawake wa Kanyaga. Aliwakumbusha kuwa wanaume wote walikuwa na sehemu za kwenda kubadilishana mawazo; kwenye bao na kilabuni. Ijapo baadhi ya wanawake walikuwa wakienda kilabuni ila walikuwa ni Wasimbe.
Hivyo aliwaomba wanawake pia watafute mradi ambao wangekuwa wakiufanya kwa pamoja ili kubadirishana mawazo huku ukiwaachia faida. Mhoja, mke wa mganga aliyeheshimika na wengi wa wanawake pale kijijini, alipendekeza pawepo na shamba kubwa la mahindi ambalo mazao yake yatasaidia kipindi cha maafa ya njaa, misiba na kadhalika. Wanawake wote walikubaliana na hoja na Malkia akatoa eneo kubwa kwa ajili ya mradi huo.
Malkia pia alipendekeza kufinyangwa kwa vyungu vya wanawake wa kijiji ili viweze kusaidia katika matukio ya sherehe na misiba. Maana kijiji kilikuwa hakina vyungu na kusababisha kipindi cha matukio ya kijamii kuazima vitu hivyo toka kwa wenyenavyo. Wakati mwingine vilikuwa vikivunjika na kusababisha hasara kwa mmiliki. Wataalamu wa kufinyanga walijitolea kuwafundisha wanawake wote kufinyanga ili kazi iwe rahisi.
Wanawake wenye uzoefu mkubwa na familia waliyamimina maalifa waliyokuwa nayo kwa wenye ndoa changa na wale wasio na uzoefu. Maswali mengi yahusuyo namna ya kuishi na waume wa ain azote yalipata ufumbuzi mkutanoni. Wale waliokuwa na uzoefu mkubwa walijitolea kuzizungukia kaya zilizokuwa zikiyumba na kuwapa mbinu madhubuti. Kipengele hiki kilikuwa na michango mingi Zaidi lakini kilipewa ufumbuzi madhubuti.
Wanawake wa Kanyaga ama kwa hakika walipanga mengi ambayo yalileta umoja na mshikamano miongoni mwao. Jioni ilikuwa ikifika hakuna mwanamke aliyekuwa akikaa upweke kwani kila mtaa ulikuwa na sehemu ya kukutania na kupiga soga au kutekeleza mradi furani. Mara kila familia ikaanza kuneemeka. Vyakula ambavyo vilikuwa adimu wanawake hawa walijitahidi kuwawina ili kila mji ukaonje chakula kile.
Baada ya mwaka mmoja kupita mafanikio yakaonekana kwenye ghala la chakula la wakina mama wa Kanyaga. Wanaume wakaanza kuwategemea na kuwaamini wake zao. Vya pombe wote wakawa wakirudi nyumbani mapema na kuacha hata kuwanyooshea wake zao vidole. Kanyaga ikainuliwa na wanawake huku wanaume wakiiba mawazo yao na kuanzisha shamba la kijiji. Ama kwa hakika mwanamke ni nguzo ya familia na jamii yake inayomzunguka.

By James Kalimanzila